![]() |
Salim Adbi pekee ndiye aliyenusurika kifo |
Taarifa kutoka mjini Mombasa pwani ya Kenya zinasema
kuwa vijana wameteketeza kanisa katika ghasia ambzo zimezuka kufutioa
kuuwawa kwa muhuburi wa kiisilamu. Inaarifiwa mtu mmoja ameuawa kwenye
ghasia hizo.
Sheikh Ibrahim Omar aliuawa kwa kupigwa risasi akiwa na washirika wake watatu.
Polisi wamesema kuwa muhubiri huyo alikuwa amehubiri katika msikiti uliohusishwa na wanamgambo wa kiisilamu wa Al Shabaab.
Haijulikani aliyetekeleza mauaji hayo ya usiku
wa kuamkia leo huku kukiendelea kuwa na hali ya wasiwasi miongini mwa
waisilamu na maafisa wa usalama mjini humo.
Sheikh Ibrahim Rogo alikuwa muhubiri katika
msikiti alipokuwa akihubiri marehemu Sheikh Aboud Rogo ambaye pia
aliuawa kwa kupigwa risasi. Aliuawa na watu wengine watatu walipokuwa
wanarejea nyumbani Alhamisi usiku baada ya kuhubiri.
Sheikh Rogo alishutumiwa kutoa mafunzo yenye
itikadi kali yaliyowashawishi vijana kujiunga na makundi ya kigaidi kama
Al Shabaab.
![]() |
Marehemu Aboud Rogo alidaiwa kuwa na uhusiano na kundi la kigaidi la Al Shabaab |
Marehemu Aboud Rogo alidaiwa kuwa na uhusiano na kundi la kigaidi la Al Shabaab
Mauaji haya ni sawa na ya marehemu Aboud Rogo Mohammed mwaka jana na ambayo yalisababisha ghasia mjini humo.
Yanakuja wiki mbili tu baada ya shambulizi la kigaidi lililofanywa dhidi ya jumba la maduka la Westgate ambapo watu 67 waliuawa
Kundi la kigaidi la al-Shabab lilikiri kufanya mashambulizi hayo ya kigaidi.
Aboud Rogo alidaiwa kuwa na uhusiano na kundi la
kigaidi la al-Shabab na baadhi ya waisilamu walioshutumu polisi
waliomuua walisema kuwa yalikuwa madai tu wala.
Ibrahim Rogo alionekana kama mrithi wa marehemu Aboud Rogo, alipohutubu katika msikiti huo.
~BBC
No comments :
Post a Comment