
Stori: MUSA MATEJA
WATANGAZAJI maarufu Bongo wa Redio Clouds Fm ya jijini Dar es Salaam,
Hamis Mandi ‘B 12’, Adam Mchomvu na Loveness Malinzi ‘Diva’, wamepigwa
chini na kituo hicho, Risasi Mchanganyiko linakupa zaidi.

Habari za chini kwa chini kutoka kwa chanzo chetu zinasema kuwa uongozi
wa Clouds umefikia hatua hiyo baada ya kuchoshwa na tabia ya utovu wa
nidhamu wa watangazaji hao.
Hata hivyo, madai ya mitaani yanasema kwamba watangazaji hao wamepigwa
chini kwa kosa la kukacha sherehe za maadhimisho ya miaka 14 ya Clouds
FM,yaliyofanyika hivi karibuni katika Viwanja vya Mwembeyanga, Temeke,
Dar.
Risasi Mchanganyiko lilimvutia waya Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji
wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba na kumwuliza juu ya ishu hiyo
ambapo alikiri.

“Ni kweli tumefikia uamuzi wa kuwasimamisha B 12, Diva na Mchomvu baada
ya kukiuka baadhi ya makubaliano baina yao na ofisi hivyo kusababisha
usumbufu mkubwa ambao ulitulazimu kuingia gharama ambazo hazikutarajiwa.
“Hatutakuwa nao kwa muda usiojulikana ingawa watu wengi wamekuwa
wakinihoji juu ya hilo lakini watachotakiwa kuelewa ni kwamba hakuna
ofisi isiyokuwa na sheria na taratibu za kuongoza watu wake, sasa hao
wamevunja taratibu zetu,” alisema Ruge bila kufafanua zaidi.
Alipoulizwa ni taratibu zipi watangazaji hao walizovunja alisema:
“Nashindwa kueleza kosa la kila mmoja ila naomba nieleweke kuwa hao
watangazaji kwa sasa tumewasimamisha kwa muda usiojulikana wakati
tukifikiria cha kufanya. Muhimu hapo ni kwamba wamekwenda kinyume na
tulivyokubaliana.”
Source -
http://www.globalpublishers.info/profiles/blogs/diva-b-12-mchomvu-out-clouds
No comments :
Post a Comment