Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi
muda huu ametangaza kuahirishwa kwa uchaguzi wa Udiwani katika kata za
Elerai, Themi, Kaloleni na kimandolu Manispaa ya Arusha hadi tarehe
14/7/2013. Amesema sababu kuu ni hali ya amani bado sio nzuri ya
kuruhusu uchaguzi kufanyika kwa sasa. Itakumbukwa kuwa Uchaguzi wa Kata
Hizi ambao ulikuwa ufanyike tarehe 16/6 uliahirishwa hadi tarehe 30/6
kutokana na mlipuko wa bomu kwenye mkutano wa kufunga kampeni wa
CHADEMA. Kampeni hazitakuwepo kwa kipindi hiki hadi tarehe ya Uchaguzi.
No comments :
Post a Comment