Top News

Friday, July 5, 2013

VIDEO: HUYU ANAWEZA KUISAIDIA CHADEMA KESI IGUNGA INAYO WAKABILI HENRY KILEO NA WENZAKE

Igunga kuna kesi.Ni kesi ya ugaidi dhidi ya Makamanda mbalimbali wa CHADEMA wakiongozwa na Kileo wa Dar. Makamanda hawa wanatuhumiwa kumteka na kumwagia tindikali Tesha-wa-Igunga. Uhalifu aliofanyiwaTesha-wa-Igunga si wa kuushabikia. Ni ukatili dhidi ya ubinaadamu.Naulaani.

Lakini, udhalimu ule aliofanyiwa usifanywe mtaji wakisiasa na kupaka matope chama fulani. Sheria zipo;vyombo vya kisheria vipo.Viachwe vifanye kazi. Hakuna haja ya viongozi wa kichama kuwa walalamikaji,washtaki,na mashahidi. Hakuna haja ya kumfanya Tesha-wa-Igunga kama lulu kwa CCM na kumtumia kuombea kura. Kufanya hivi, ni kufilisika kisiasa.

CHADEMA,wakati wenu ni huu. Jilindeni dhidi na mnayoyadai kuwa ni 'mafilamu' ya chama tawala. Pamoja na kuwa na Mawakili wasomi wenye weledi,bado mnahitaji mashahidi. Mashahidi wanapatikana Igunga.Mmojawao ni kijana (aliyewahi kuwekwa Youtube yake humu) ambaye alihama toka CCM kwenda CHADEMA. Kijana huyu alisema jambo juu ya Tesha-wa-Igunga.

Alisema kuwa Tesha-wa-Igunga amemwagiwa tindikali nawana-CCM wenzake ambao aliwadhulumu pesa zao za posho ya kampeni. Kijana huyu atafutwe,alindwe na atumike kama shahidi. Kwa wafuatiliaji wa Igunga watakubaliana nami kuwa wakati wa kampeni filamu ilianza kutengenezwa. Ikadaiwa kuwa CHADEMA walivamia nyumba fulani na kuiteketeza kwa moto. Cha kushangaza,viliungua vitu vyote pamoja na nyumba husika lakini kuna kitu kikabaki.

Ni kitu kilichotarajiwa kuungua mapema kuliko vingine.Karatasi. Eti, ilibaki karatasi (kipeperushi) kilichodai kuandikwa kwa tambo na CHADEMA kuwa wao ndio waliochoma nyumba hiyo. Ngumu kuamini.

Kamanda Kileo na wenzake wanaimani na kuisubiri CHADEMA.Wamejawa matumaini ya kuoshwa dhidi ya kesi yao na kurudi ulingoni kupambana kisiasa. Kamanda Kileo na wenzake wanatamani kupata ushindi wa ki-Lwakatare. Amini nawaambieni, ipo siku Tanzania itakuwa na siasa safi na za ushindani!

No comments :

Post a Comment

Designed By ApexbnewZ