Top News

Tuesday, October 1, 2013

CUF, CHADEMA na NCCR Mageuzi waendelea kutangaza hali ya hatari tarehe 10 Mwezi huu.




MUUNGANO wa vyama vitatu vya upinzani umesema kuanzia sasa haupo tayari
kubatilisha kusudio lao la kufanya maandamano nchi nzima kwa kukutana na
kiongozi yeyote isipokuwa tu Rais Jakaya Kikwete atapotangaza kutosaini
muswada uliopitishwa bungeni kinyemela. Pia umesema hautakubali kamwe
kuzuiwa na chombo chochote kufanya maandamano na mikutano ifikapo Oktoba
10 mwaka huu.

Hayo yalisemwa Dar es Salaam jana na Viongozi wa Kamati ya Ufundi ya
Muungano wa vyama vya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),
Chama cha Wananchi (CUF) na NCCR-Mageuzi.

Hao ni Mkurugenzi wa
Habari na Uenezi wa Chadema, John Mnyika, Mkuu wa Idara na Taasisi za
Dola na Vyombo vya Uwakilishi NCCR Mageuzi, Faustine Sungura na Naibu
Mkurugenzi wa Habari na Haki za Binadamu na Uhusiano wa Umma kutoka CUF,
Abdul Kambaya.

Mnyika alisema uamuzi huo umefikiwa kwa pamoja
na wenyeviti wa vyama hivyo vitatu kwamba muda uliobaki sasa hadi
kufikia Oktoba 10 mwaka huu ni wa kukutana na makundi maalumu kuwaeleza
kasoro zilizopo kwenye mswada na kuwashawishi kuwaunga mkono.

“Tunapenda
kuwaeleza vyama vitatu tayari vimekamilisha maandalizi ya kufanya
mikutano nchi nzima, tumejipanga kupinga Rais Kikwete kusaini muswada
huo kwa njia mbalimbali zikiwamo za demekrasia, maandamano na raia.

“Jambo
hili ni kubwa na lina maslahi kwa kila Mtanzania, hivyo tunaomba kila
kundi na taasisi ziungana na sisi na kufanya maandamano kwa njia ile
watakayoona inafaa na hata kufanya mgomo.

“Viongozi wa dini
wanaweza kuandaa sala ya kuliombea taifa kupinga Rais Kikwete kutosaini
muswada huo, hivyo hivyo katika taasisi nyingine kulingana na nafasi
zao, nasema siku hiyo itakuwa ni ya kupinga kila kitu.

Kama
ikitokea kundi linazuia mikutano hiyo au maandamano hayo kwa kusema tii
sheria bila shuruti, kamwe mtu asikubali kuzuiwa, yaani tunataka siku
hiyo iwe ya kupinga kila jambo litakalijitokeza kwa lengo la
kukwamisha,alisema.

Abdul Kambaya kutoka CUF, alisisitiza
kumuomba Rais Kikwete kutosaini muswada huo na badala yake kuurudisha
bungeni kuufanyia marekebisho ambayo yanalalamikiwa

-Mtanzania

No comments :

Post a Comment

Designed By ApexbnewZ