Top News

Sunday, July 28, 2013

Ha ha ha Dah Mbavu zangu! Kama jumapili yako haijakaa powa basi Unaweza Cheki hapa

Mtoto: Baba nitumie hela ya matumizi huku shule hali ni mbaya la sivyo nitajinyonga.
Baba: Huku nyumbani hli ni mbaya kuliko huko shuleni, kwa hiyo kama unajinyonga sawa tu kwa sababu utapunguza bajeti. Kopa kamba dukani ntakuja kulipa nikija kuchukua maiti yako. Mungu akulaze mahali pema peponi mwanangu.

 MC anamsifia Bi. Harusi
"Sasa nawapa sifa kubwa ya Bibi harusi. Tangu namfahamu huwa havai nguo za ndani!"
Watu wakaduwaa
MC "Narudia tena kwa msisitizo na sijakosea. Bi. Harusi huyu huwa havai kabisa nguo za ndani. Yeye anavaa za kutoka Italy, England na USA. Si za Tanzania. Hebu mshangilieni!"
Kila mtu "Ahaaaaaa...!"

 MPARE NA PESA
Binti: Mama, nimemuomba baba hela ya saluni akaninyoa nywele
Mama: Una bahati sana mwanangu. Ungemuomba hela ya whitedent angekung'oa meno!

 UWONGO HAUFAI
Jamaa: Unasoma?
Demu: Hapana sisomi, vipi wewe unasoma?
Jamaa: Ndo nipo form 4 Jangwani
Demu: Jamani hiyo si shule ya wasichana?
Jamaa: Ah! sorry nimechanganya nipo Kisutu
Demu: Mwee mbona nayo ya wasichana
Jamaa: Haa! Nilikuwa nakutania nachukua PhD IFM
Demu: Mh! Ina maana IFM imeanza kutoa PhD?
Jamaa: Ishia zako. Demu mwenyewe hulipi wala nini! Unauliza maswali kama tupo uhamiaji? KWA TAARIFA YAKO NACHUKUA DEGREE YA UDAKTARI CBE!

 Mlevi kaanguka toka ghorofani fasta watu wakamfata kumsaidia wakamuuliza VIPI IMEKUAJE? Mlevi akajibu: "HATA SIJUI NA MIE NDO NAFIKA SASA HIVI..."


No comments :

Post a Comment

Designed By ApexbnewZ