
BAADA ya kukamatwa na dawa za kulevya nchini Afrika Kusini, msanii
anayeshiriki katika video za wasanii wa muziki wa bongo fleva, Agnes
Jerald 'Masogange' na mwenzake Melisa Edward, ukweli umeibainika kwamba
dawa walizokamatwa nazo ni za kutengenezea dawa za kulevya, ambazo
hazipatikani nchini na hazina matumizi yoyote.
Kupitia taarifa
rasmi zilionesha kuwa, Chemical bashirifu ndiyo aina ya dawa
walizokamatwa nazo nchini humo, ambapo wasanii hao walikamatwa nchini
Afrika Kusini wakitokea Tanzania.
Akizungumza ofisini kwake Dar
es Salaam leo Kamishina wa Tume ya Kuratibu na Kuthibiti Dawa za Kulevya
nchini, Christopher Shekiondo alisema kwamba kwa mujibu wa sheria za
nchi, dawa walizokamatwanazo wasichana hao zinatumika kutengenezea dawa
za kulevya, ambapo adhabu yao ni sawa na mtu aliyekamatwa na dawa za
kulevya.
Wasichana hao walikamatwa Julai 5, mwaka huu nchini humo
wakiwa shehena ya dawa za kulevya zenye thamani ya sh. bilioni 6.8
wakitokea Tanzania.
Shekiondo alisema dawa walizokamatwa nazo
hazitumiki moja kwa moja kama dawa, bali zinatumika kutengenezea dawa za
kulevya hivyo kwa mujibu wa sheria, adhabu zao zinakwenda sambamba na
waliokamtwa na dawa za kulevya.
"Dawa hizo hazitumiki moja kwa
moja bali zinatumika kutengenezea dawa za kulevya, hivyo kama taarifa
tulizopata ni sahihi juu ya aina ya dawa walizokamatwa nazo na dawa hizi
hazitumiki sana nchini, bali zinatumika Afrika Kusini, Asia pamoja na
Ulaya," alisema Shekiondo.
Alisema kwa mujibu wa sheria za nchi,
mtu anayekamatwa na dawa hizo mara nyingi hukumbwa na adhabu ya
kuhukumiwa miaka 20 au kifungo cha maisha.
Akielezea kuhusu
wasichana hao wawili kupanda kizimbana juzi, Kamishina huyo aliweka wazi
kuwa hadi sasa hawajapata taarifa zozote rasmi, zaidi ya kupokea zile
za awali za kushikiriwa na Jeshi la Polisi Afrika Kusini kwa ajili ya
uchunguzi.
Kamishina huyo alisema inaonesha Watanzania wengi
wamekamatwa na dawa za kulevya nchini Brazil ambao idadi yao inafikia
109, ambapo wengi wao wameshahukumiwa.
Alisema watu hao
wamekamtwa nchini humo, wakiwa na dawa aina ya cocain kwa ajili ya
kusafirisha nchi nyingine, huku baadhi yao wamehukumiwa kunyongwa pamoja
na kifungo cha maisha, ingawa idadi kamili ya watu hao bado haijafika
rasmi.
"Tumepokea taarifa jumla ya Watanzania 109 wamekamtwa
nchini Brazil, ingawa bado tunasubiri kujua ni wangapi waliohukumiwa
kifo, pamoja na kifungo cha maisha," alisema Shekiondo.
Aliongezea
kuwa baadhi ya nchi nyingine, ambazo Watanzania wanakamatwa na dawa
hizo za kulevya wakiwa wanasafirisha ni China vijana 34, Kenya 30,
Pakistani 16, Falme za Kiarabu ikiwemo Dubai 14, pamoja na nchi nyingine
kama Japan, Argentina, Msumbiji, Afrika Kusini, Ureno, pamoja na
Uingereza.
Akizungumzia hukumu ambazo zimeshatolewa baadhi ya
nchi walizokamatwa Watanzania hao,, Kamishina huyo alisema Brazil ambayo
ndiyo Watanzania wengi wamekamatwa idadi kamili, bado hawajapata ingawa
Kenya tayari wapo waliohukumiwa kifungo cha maisha, huku wengine wakiwa
wamehukumiwa kifungo cha miaka 20 hadi 40, nchi China wapo
waliohukumiwa kifo na kifungo cha maisha.
Shekiondo alisema Tanzania kwa sasa inajulikana kama ni njia ya kusafirisha dawa hizo.
Alisema
kuna baadhi ya watu wanatumia maji kusafirisha dawa hizo, yaani meli,
jahazi pamoja na mitumbwi, hivyo wana mikakati ya kutoa elimu kwa jamii
kuhusu udhibiti wa matumizi ya dawa za kulevya.
Read more ...