Top News
Showing posts with label Habari. Show all posts
Showing posts with label Habari. Show all posts

Saturday, November 2, 2013

Lema aibua mazito ndani ya chadema ni kuhusu WASALITI na WANAFIKI ndani ya CHADEMA... Zitto , Shibuda wahusishwa


Safari yetu ya kubadilisha utawala inaonekana kufika ukingoni na nifuraha ya kila Mtu mwenye hisia ya ukweli katika maisha na ninapotazama mbali sana ninaona jinsi ambavyo Usaliti na Unafiki unavyoangamiza Taifa ni bahati mbaya sana uwezi kuwaepuka katika harakati hizi lakini tukiwa makini tunaweza kuwathibiti .

Kama Chadema leo itashindwa kuwachukulia hatua wasaliti wa wazi wa kazi hii njema ni vipi Chadema itaweza kuitaka Serikali na Rais iwajibishe Viongozi wake katika ufisadi na wizi wa mamilioni ? Na Wananchi lazima wajue lengo kubwa na muhimu la Chadema kwanza liwe kubadilisha fikra na mitazamo na kuupa UMMA elimu na mamlaka na nguvu ya kusimamia Taifa lao katika kuhoji ,kudadisi na kukemea , kwani UMMA usipojua wajibu wake katika kusimamia rasilimali na Taifa lao , ukweli utabaki kuwa Nchi itabadilishwa na kufanikishwa na Jamii iliyoamua kuishi matendo dhahiri ya ukweli na haki na sio unafiki na usaliti .

Viongozi wote wa Siasa wanatokana na Jamii kwa hiyo jamii Thabiti inayo furahia UTU ni Nchi bora tutakayoijenga lakini Jamii yenye woga na hofu na Sifa itazaa Taifa lenye usaliti na Wanafiki . Usaliti na Unafiki unaliangamiza Taifa sana . Maombi na Dua za Watu wengi kuelekea 2015ni kutaka kuona Chadema inachukua Nchi , lakini Dua na Sala hizi zina Imani kubwa na Viongozi wa Chadema na sio rangi ya Chadema , hivyo ni muhimu Chadema kuchukua hatua sasa ya kusafisha Chama na kama hatua hiyo muhimu ya kuondoa Watu wenye rangi mbili italeta madhara katika Uchaguzi Mkuu wa 2015 kwamba tunaweza tusishinde dola basi madhara hayo ni muhimu kwani lengo letu lisiwe tu kwenda Ikulu bali kubadilisha fikra ya utawala katika kutenda na kuamua .

“ Ni bora Simba wakali mia moja walioko Nje kuliko nyoka mdogo mmoja aliye ndani “ Chadema lazima ifanye maamuzi sasa ya kusafisha Nyumba yake la sivyo itakuja kujuta katika siku za mwisho , wasaliti wote waondolewe hasa yule Kiongozi wao kwani hakuna genge la usaliti lisilokuwa na Kiongozi , kuna Watu wengi Vijana wamekuwa wahanga na ndoto zao kupotea katika Siasa kwa sababu waliongozwa vibaya na Kiongozi mkubwa anayeratibu usaliti ndani ya Chama .

Mtu huyu wote tunamjua ni matumaini yangu Usaliti wake sasa utafika kikomo kama Chama kitaamua kuwa na busara za kutosha katika kujenga siku njema zinazokuja . Mtu huyu amefanya mambo mengi mabaya katika Chama yanayohusu usaliti na amewaponza Vijana wengi na kuangamiza ndoto zao kwa sababu ya mambo yake binafsi .

“ To me, the thing that is worse than death is betrayal. You see, I could conceive death, but I could not conceive betrayal.” Malcolm X
Lema Godbless - Mp
Read more ...

Wednesday, October 16, 2013

Ujumbe Aliouandika Ney Wamitego Instagram Unatisha.


Mpaka sasa ney haja sema ni nani na nini kimepelekea yeye kuandika hivi kuhusu maisha yake ya muziki. Ila inaonyesha hapa kati amekutana na misuko suko kwenye ,mishe zake, kuchukiwa na kutokukubalika kunaweza pelekea mtu kusema yote haya.
Bonyeza Read More Kuona Ujumbe Huo

Read more ...

Tuesday, October 15, 2013

Nisher na Lucci waandika historia nyingine kwa video ya Sumu

Jikubali ya Ben Pol ilikuwa ni video ya kwanza aliyoongoza Nisher kuchezwa Channel O, na sasa muongozaji huyo wa video kutoka Arusha, ameandika historia nyingine na video aliyomfanyia producer wa Transformax, Lucci Da Don.

Video hiyo imekuwa video ya kwanza ya Nisher kuwahi kukubalika na kuwekwa kwenye mtandao wa Marekani wa ViewHipHop.
“Nimefurahishwa na mapokezi ya video mpya ya #SUMU by #LUCCI… Kwa mara ya kwanza katika video zangu zote, video hii imefaulu kukubalika katika blog moja ya Marekani Kwa jina la “VIEWHIPHOP” yenye followers 43,336,” aliandika kwenye Facebook.

Video ya Lucci imewekwa kwenye video za wasanii ambao hawapo chini ya label yoyote (unsigned).
Read more ...

Sunday, October 13, 2013

Taarifa kuhusu mwandishi wa ITV Ufoo Saro kujeruhiwa kwa risasi

Rais Jakaya Kikwete akiwa na Ufoo Saro
Mwandishi wa ITV Ufoo Saro amejeruhiwa kwa risasi iliyopigwa na mwanaume mmoja alieripotiwa kutokua na maelewano mazuri ambapo kwenye hili tukio mwanaume huyu alimpiga risasi na kumuua mama mzazi wa Ufoo Saro.

Mwanaume huyu alimpiga Ufoo risasi mbili ambazo zilimjeruhi na kudhani kwamba amemuua na kisha yeye mwenyewe kujipiga risasi na kufariki.

Mambo yote haya yalitokea huko Kibamba ambapo taarifa zisiso rasmi zinasema kwamba huyo mwanaume baada ya kuwa na ugomvi kati yake na Ufoo, alienda kuongea na mama mzazi wa Ufoo baada ya kuona mama yupo upande wa Ufoo ndio akaamua kuua.

Read more ...

Saturday, October 12, 2013

Maskini!: HOUSEGELI Amnyonga mtoto nakumtupa kwenye dibwi la maji machafu



Hausigeli aliyejulikana kwa jina moja la Ester (14) yupo matatani kwa madai ya kumuua mtoto Arafat Allan (3) kwa
kumnyonga shingo na kumpiga na kitu kizito kichwani kisha kuutumbukiza mwili wake kwenye dimbwi la maji machafu.

Tukio hilo lilijiri Jumapili iliyopita Mailimoja, Kibaha mkoani Pwani ambako marehemu alikuwa akiishi na wazazi wake.

Akizungumza kwa uchungu, mama mzazi wa mtoto huyo, Zakia Peter ambaye amelazwa katika Zahanati ya Kellen kutokana na mshtuko wa kifo cha mwanaye, alisema siku ya tukio, hausigeli huyo aliyekuwa na siku mbili tangu
aanze kazi aling’ang’ania kutumwa sokoni saa mbili asubuhi ambapo alimkubalia na kumuagiza mboga.

AONDOKA NA MTOTO
Bila mwanamke huyo kujua, msichana huyo alimpitia
Arafat kwa jirani alikokuwa akicheza na wenzake na kuondoka naye kwa madai anamsindikiza.
  
“Nilipoona muda unasonga mbele bila hausigeli kurudi na mtoto nilianza kuwatafuta,” alisema mama wa marehemu.
Akasema aliwatafuta kwa muda mrefu bila mafanikio mwishowe yeye na majirani zake wakaenda kutoa taarifa polisi na kufunguliwa jalada la kesi
KB/RB/1154/2013 TAARIFA.


HABARI ZASAMBAA MAITI YA MTOTO KUONEKANA KWENYE DIMBWI LA MAJI
Mama wa marehemu aliendelea kusema kuwa zoezi la kumsaka msichana huyo na mtoto wake liliendelea mpaka Jumanne iliyopita ambapo habari zilisambaa kwamba kuna maiti ya mtoto wa kiume  imekutwa ikielea kwenye dimbwi la
maji machafu linalotumika kumwagilia bustani za mboga maeneo hayo.
  
“Niliondoka na ndugu wengine hadi kwenye dimbwi hilo! Nilipata mshtuko mkubwa kukuta maiti ya mtoto anayeelea ni ya mwanangu Arafat,” alisema huku machozi yakimtoka.

MADAKTARI WAANIKA RIPOTI YA UCHUNGUZI
Baada ya hapo, mwili huo ulipelekwa katika Hospitali Teule ya Tumbi, Kibaha ambapo madaktari waliufanyia uchunguzi na kubaini kuwa marehemu alinyongwa shingo na kupigwa na kitu kizito kichwani hali iliyomsababishia mauti.

MAUAJI YAHUSISHWA NA USHIRIKINA
Baadhi ya watu waliozungumza nasi   akiwemo mama wa marehemu, walisema kwa siku mbili hizo alizofanya kazi hausigeli huyo alionekana kuwa na mambo ya kishirikina kwani asubuhi ya siku ya tukio aliamka akiwa amenyolewa
nywele upande mmoja.
  
“Siku hiyo ya Jumapili huyo mdada wa kazi aliamka akiwa amenyolewa nywele upande mmoja, alipoambiwa amalizie zote alikataa akisema atanyoa baada ya kutoka sokoni ambapo hakurudi tena,” alisema mama wa marehemu.

HAUSIGELI AKAMATWA
Jumatatu iliyopita, siku moja baada ya tukio, hausigeli huyo alikutwa akirandaranda stendi akiomba fedha za nauli ili
arudi kwao Mbeya lakini alikamatwa na kufikishwa kwenye kituo kidogo cha polisi.

Habari zinasema hali kwenye kituo hicho ilikuwa mbaya
kufuatia baadhi ya wakazi wa eneo hilo kujaribu kukivamia ili wamuue mtuhumiwa huyo. Ilibidi mtuhumiwa ahamishiwe Kituo cha Polisi cha Tumbi,Kibaha.

MANENO YA WATU WA KARIBU
Kwa mujibu wa watu wa karibu wa familia hiyo, msichana huyo aliokotwa na ndugu wa baba wa marehemu baada ya
kumkuta barabarani akiomba msaada akidai anateswa na ndugu zake, wakampeleka kwa baba wa marehemu ili wamsaidie ambapo walimpa shughuli ya kazi za ndani.

Baba wa marehemu, Allan hakuweza kuzungumza
kutokana na kuwa kwenye hali mbaya katika Zahanati ya Kellen alikolazwa baada ya mwanaye kuzikwa katika Makaburi ya Mailimoja, Jumatano iliyopita.

-GPL

Read more ...

Devota Mbaga: Huyu ndio msanii wa bongo Movie Alie vuliwa nguo uwanja wa ndege china

 
Devota Mbaga kushoto
MSANII wa Bongo Movie, Devota Mbaga hivi karibuni alipatwa na kisanga cha mwaka baada ya kuvuliwa nguo na maofisa wa uhamiaji alipoenda Hong Kong, nchini China kwa ajili ya shughuli zake za kibiashara.Kwa mujibu wa staa huyo, alifanyiwa kitendo hicho cha kuvuliwa nguo zote na maofisa wa uhamiaji mara alipotua Uwanja wa Ndege wa Hong Kong na kumsachi kwa kuhofiwa kuwa amebeba ‘unga’.
 
Akizungumza na mwandishi wetu kwa njia ya simu, Devota alisema baada ya kuvuliwa, alishikwa sehemu zake za siri kitendo alichokiita ni cha kidhalilishaji.
 
“Ilikuwa ni baada ya kugongewa pasipoti yangu nikaingizwa kwenye kitengo cha polisi wa madawa ya kulevya ambao walinitaka nivue nguo zote ili nikaguliwe,” alisema kwa masikitiko.
 
Msanii huyo alisema mbaya zaidi siku hiyo alikuwa katika mzunguko wake wa mwezi lakini maofisa hao hawakujali.
 
Kama vile haitoshi, Devota alisema kuwa, baada ya kumalizika kwa zoezi hilo maofisa hao walimchezea sehemu za kifuani huku wakimwambia kama hakutaka kufanyiwa hivyo angerudishwa alikotoka.
 
 “Kwa kweli nimeumia sana kwa kitendo nilichofanyiwa, nimeshinda nikilia kutwa nzima na kila nikikumbuka naumia,” alisema Devota.
Read more ...

Thursday, October 10, 2013

Zitto Kabwe Ataja Mshahara anaolipwa waziri mkuu kwa Mwezi

HATIMAYE Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Zitto Kabwe, ameweka wazi mshahara wa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.

Zitto ameutaja mshahara huo wa Pinda anayejitambulisha kama ‘mtoto wa mkulima’ juzi mjini Mpanda na jana wilayani Sikonge wakati akihutubia mikutano ya hadhara katika ziara ya Kanda ya Magharibi kwa ajili ya ujenzi wa chama.

Alisema Pinda anapokea jumla ya sh milioni 26, ambazo ni kiasi kikubwa kulinganisha na uchumi wa nchi.

Akichanganua alisema Pinda anapokea sh mil. 11.2 kama mbunge, sh mil. 8 kwa nafasi ya waziri na kiasi kinachosalia kufikia sh mil. 26 kwa nafasi yake ya uwaziri mkuu.

Alisema sababu hiyo ya mishahara mikubwa isiyokatwa kodi ndiyo huwafanya viongozi wa serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa wakali pale vyombo vya habari vinapotaka kuwafahamisha wananchi namna watumishi wao wanavyojilipa.

“Nimeanza na mshahara wa waziri mkuu pia siku zijazo nitataja na wa rais, kwa kuwa amesaini makubaliano na Serikali ya Marekani kuendesha nchi kwa uwazi, na moja ya uwazi ni kwa muajiri kujua kiasi anachomlipa mwajiriwa wake,” alisema Zitto.

Hatua ya Zitto imekuja baada ya kuwapo mvutano mkubwa kuhusiana na kile kinachodaiwa ‘usiri’ wa mishahara ya watumishi wa umma, wakati ni haki ya walipa kodi kujua kile wanachowalipa walioomba kuwaongoza.

Kodi ya laini za simu

Akizungumzia sakata la kodi katika laini za simu, Zitto alisema CCM ina ajenda ya kisiasa kwa ajili ya uchaguzi wa mwaka 2015.

Alisema serikali baada ya kubaini watu wengi wanapeana taarifa kwa njia ya ujumbe mfupi, hususan katika masuala ya kisiasa, wakaona njia sahihi ya kudhibiti ni kuwatoza kodi ya laini ili kupunguza hatari ya mawasiliano hayo kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu ujao.

“Sikuwepo bungeni wakati wabunge wa CCM wanapitisha kadhia hiyo ya kuwanyonya wananchi, wenzangu wakaniambai tukasema hapana, kwa maana tuliona hii leo kuna Watanzania wengi wasio na uwezo wa kuhudumia simu kwa kiasi cha sh 1,000 kwa mwezi,” alisema Zitto.

Akijibu maswali ya wananchi mjini Mpanda waliotaka kujua sababu ya kupunguza makali bungeni, Zitto alisema hakuna makali yaliyopungua bali ni mitazamo ya watu.

Alisema kwa kushirikiana na wabunge wenzake wa upinzani wamekuwa wakisimamia hoja zenye manufaa kwa wananachi huku wabunge wanaojipambanua kuwa majasiri kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakiwaunga mkono wazi wazi.

Akiwa  wilayani Sikonge, Zitto alisema Watanzania hawawezi kujivunia uhuru huku mama zao, watoto wao na wazee wao wakiwa hawana uhakika wa kupata huduma bora ya afya, elimu na maji safi.

Alisema kwa sasa Tanzania ni taifa moja lililogawanyika katika nchi mbili za wenye fedha na wasio na fedha.


Alisema nchi ya wenye fedha, familia zao husoma katika shule bora, zenye mazingira bora na walimu wazuri, hutibiwa katika hospitali zenye hadhi na huduma muhimu na ikibidi nje ya nchi, huku nchi ya wasio na fedha  familia zao wakiishi kwa shida, kusoma katika majengo ya shule na walimu wasiopata mishahara ya kuridhisha na hospitali zisizokuwa na huduma muhimu licha ya kuchangia kiasi cha fedha kwa ajili ya bima ya afya.
Source:Tanzania Daima
Read more ...

Sunday, October 6, 2013

Zitto Kabwe awasilisha muswada binafisi wakufuta sheria ya magazeti ya mwaka 1976




Napenda kuujulisha umma kwamba leo ( Ijumaa tarehe 4  ) Oktoba, 2013 nimewasilisha kwa Katibu wa Bunge muswada binafsi Bungeni kufuta Sheria ya Magazeti yamwaka 1976.
Changamoto iliyopo ni Sheria mbadala ya vyombo vya habari baada ya Sheria ya sasa kufutwa. Hata hivyo wadau wa habari kama Baraza la Habari Tanzania wameshafanyia kazi suala hili kwa muda mrefu sana na wana mawazo kuhusu sheria mbadala. Nimejulishwa kuwa muswada wa sheria mpya ya habari tayari upo. 
Kwa hiyo katika mchakato wa kujadili muswada binafsi wa kufuta sheria ya magazeti ya mwaka 1976 mabadiliko yanaweza kufanywa ili kutunga sheria mpya. Hatua ya kwanza ni kuifuta sheria hii kandamizi ambayo kiukweli

tumechukua muda mrefu sana na baada ya madhara makubwa kufikia hatua ya muswada wa kuifuta.
Nimeamua kutumia njia za kawaida za kuwasilisha muswada na kuepuka njia ya dharura ili kujenga mazingira ya wadau wa habari kushiriki vya kutosha katika mabadiliko yanayotakiwa. Njia ya dharura ni ya haraka lakini huziba fursa za kupata maoni ya wadau ambao kimsingi ndio wenye sheria yenyewe haswa. 
Hivyo nimepeleka muswada leo ili uchapwe kwenye gazeti la Serikali (GN) kwa mujibu wa kanuni za Bunge, kisha usomwe kwa mara ya kwanza, uende kwa wadau kwa mjadala na marekebisho na kisha kusomwa kwa mara ya pili na kupitishwa na Bunge.

Ikumbukwe kuwa juhudi za kufuta sheria hii ni juhudi za wadau wa tasnia ya habari na ni juhudi walizofanya kwa muda mrefu sana. Mimi kama Mbunge ninawasilisha tu kwa sababu taratibu zetu za kuandika sheria zinataka ama Serikali, 
Kamatiya Bunge au Mbunge kuwasilisha muswada. Kwa muda mrefu tumewaangusha wana habari kwa kutosukuma vya kutosha mabadiliko waliyokuwa wanayapigania. Hata hivyo, kuna msemo wa kihindi 'asubuhi huanza pale unapoamka'. Sasa tuchukue hatua za kufuta sheria hii kandamizi. 

 Zitto Kabwe,Mb
Kigoma Kaskazini

Read more ...

Picha: Mzuka wa wakazi wa Moshi ndani ya Serengeti Fiesta Ni balaa "Moshi yafunika"

115 
Shilole kama kawaida
114
113
112 
Shilole akiwa kazini baada ya kutoa mwaliko wa kudance na shabiki
1 
Juma Nature na timu yake..
2 
Chege na Temba
3
101 
Godzilla…
107 
Cassim Mganga
106 
Young Killer Mwanza Mwanza
105
104
103 
Stamina…
102 
Kingzillah…
108 
Mr Blue
109
110
111
116
Ay
117
Mwana FA
118
119
120
121
123
124
125
126
J Martins wa Nigeria nae alikuwepo kufanya showa mbapo kama ilivyotekea kwa show yake ya kwanza ya Fiesta pale 96.0 Tanga, J aligawa zawadi kwa fans aliowaita yeye mwenyewe kwenye stage…. Tanga aligawa cheni pamoja na pesa na Moshi kagawa saa na pesa kwa mashabiki wawili tofauti.
127
128
131
132
130
135
Weusi kwenye stage
134
Hii picha ya juu na ya chini ni shangwe walilopigiwa Weusi wakati wakiwa kwenye stage
133
136 
Dullysykes…
137
138
Rich Mavoco
139
Jambo Squad… Mamong’o
140
Show ilihostiwa na B12 na Dj Fetty kutoka XXL ya Clouds FM.
141
Ney wa Mitego
142
Linah Sanga…
145
146
Christian Bella…
147
Menina akiwa backstage baada ya kufanya show…
149
Ally Nipishe
143 
Mmetisha watu wangu wa nguvu Moshi…. hongereni kwa kumaliza ticket aisee! daaah
144
150
148
129
Read more ...
Designed By ApexbnewZ