Top News
Showing posts with label Diamond Platinuamz. Show all posts
Showing posts with label Diamond Platinuamz. Show all posts

Wednesday, July 30, 2014

Picha: Mapokezi ya Diamond Platinum Kutoka AFRIMAMA Marekani.

MWANAMUZIKI wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, leo amepokelewa na msafara kama wa rais na watu wa maeneo alikozaliwa Tandale jijini Dar baada ya kushuka kwenye ndege akitokea kwenye tuzo za Afrimma zilizotolewa nchini Marekani. Picha na GPL
Diamond akiwa juu ya gari akiwa ameshikilia tuzo aliyopata.
Watu mbalimbali wakitembea kwa miguu katika msafara huo kumpokea shujaa wao.
Akiwa kwenye picha ya pozi na tuzo yake.
Watu mbalimbali wakiwa wamelizingira gari la Wema wakimtaka atoke nje, lakini hakutoka.
Waendesha bodaboda wakiongoza msafara huo.
Read more ...

Monday, July 28, 2014

Diamond na Lady Jay Dee Washinda Tuzo za AFRIMAMA 2014 zilizofanyika marekani

Kwa mara nyingine Diamond Platnumz ameendelea kuipeperusha vizuri bendera ya Tanzania kimataifa, baada ya kushinda tuzo ya AFRIMMA 2014 (African Muzik Magazine Awards) zilizofanyika July 26, Eisemann Center Richardson, Texas, Marekani. Diamond ameshinda kipengele cha mwanamuziki bora wa kiume Afrika mashariki.
d afrimma
Diamond muda mfupi baada ya kupokea tuzo yake
Mtanzania mwingine aliyeing’arisha Tanzania katika tuzo hizo ni Lady Jaydee, ambaye nae ameshinda tuzo moja ya mwanamuziki bora wa kike Afrika mashariki.
Diamond kupitia Instagram amepost picha akiwa na tuzo yake na kuandika:
“First of all napenda nimshkuru sana Mwenyez mungu, Mama, Family, My management, kipenzi changu, Media, bila kuwasahau nyinyi mashabiki zangu pendwa kwani sikuzote mmekuwa mkinisupport bega kwa bega kwenye shida na raha…Niwashkuru pia Wasanii wenzangu toka nje na ndani ya Tanzania kwani naamini changamoto tunazopeana ndio zimefanya hadi sasa mziki wetu ufikie hapa…hakika tunzo hizi si zangu bali ni za Muziki wa Bongo flavour… Mwisho kabisa nimshkuru Mh Rais Jakaya Mrisho kikwete kwa mchango wake wa kila siku katika sanaa yetu!… Mr President your Son Did it!!!!! #MdogMdogo”.



Naye Lady Jaydee ameandika:
Nashukuru wote mnaokubali kazi zangu, wote mnaosimama na kutetea JayDee bila kusita, nashukuru kwa Tuzo nyingine tena toka AFRIMMA . Wahenga walinena kuwa utavuna ulichopanda, mapenzi tele kwa kila mtu.

Share
d n d afrimma Diamond na Davido baada ya kupokea tuzo zao
Wanamuziki wengine walioshinda ni pamoja na Davido na Flavour wa Nigeria, ambao wamenyakua tuzo mbili kila mmoja.
Nchi ya Nigeria ndio iliyong’ara zaidi kwa kupata jumla ya tuzo kumi, ikifuatiwa na Afrika Kusini ambao wamepata tuzo tano.
Hii ni orodha kamili ya washindi wa AFRIMMA AWARDS 2014
Best DJ Africa 2014- Dj Black (Ghana)

Best African DJ USA 2014 – Dj Josh (Kenya)

Best Video of the Year 2014- Flavour (Nigeria)
Best Male East Africa 2014- Diamond (Tanzania)

Best Male West Africa 2014- Davido (Nigeria)
Best Female East Africa 2014- Lady Jaydee (Tanzania)

Best Female West Africa 2014 – Tiwa Savage (Nigeria)

Best Male Central Africa 2014 – Fally Pupa (Congo)

Best Female Central Africa 2014- Gasha ( Cameroon)

Best Male Southern Africa 2014- Khuli Chana (South Africa)

Best African Group 2014- P-square (Nigeria)

Best Male Diaspora 2014- Fuse ODG (Ghana)

Best Female Diaspora 2014- Les Nubians (Cameroon)

Best Female Southern Africa 2014- Zahara (South Africa)

Best Dancehall Artist 2014 – Timaya (Nigeria)

Best Dance in a Video 2014- Iyanya (Lekwa Ukwu) (Nigeria)

Best Gospel Artiste 2014- Bahati (Kenya)

Best Traditional Artist 2014- Flavour (Nigeria)

Best Newcomer 2014- Stanley Enow (Cameroon)

Best Video Director 2014- Ogopa Dj’s (Kenya)

Music Producer of the year 2014- Dj Oskido (South Africa)

Best Dance Group 2014- Imagineto (Nigeria)

Best Rap Act 2014- Sarkodie (Ghana)

Best Collaboration 2014- Mafikizolo ft Uhuru (Khona) (South Africa)

Song of the Year 2014- Kcee (Nigeria)

Artist of the Year 2014- Davido (Nigeria)

Leadership in Music Award 2014- 2face Idibia

Legendary Award 2014- Yvonne Chaka Chaka

Transformational Leadership Award 2014- Chief Dr. Godswill Akpabio
Read more ...

Friday, November 1, 2013

Vita ya Rich Mavoko na Diamond Platnumz kwenye Music yaiva Mavoko amfungukia Platnumz

Hitmaker wa Roho Yangu, Richie Mavoko amesema anajua kile ambacho Diamond Platnumz anawashikia watu, na yeye anajua kipi cha kufanya, ndio maana anaonekana kuwa tishio kwake.
page
Akiongea , Richie Mavoko amesema alianza kumsikia Diamond tangu akiwa shule na kwamba hakatai kuwa kuna vitu alijifunza kutoka kwake.

“Mimi Diamond anatoka, mimi nipo shule, kwahiyo kuna vitu vingi nimeviona, labda yeye amepitaje, amekosea nini na mimi nifanyeje ndio maana mara nyingi mimi naonekana noma kwasababu mimi nishajua wao wanataka nini. Yaani mimi nishajua anapowashkia watu halafu mimi nshajua natakiwa nifanye nini,”alisema.
Mavoko aliendelea kudai kuwa muziki wake na wa Diamond haufanani hata kidogo. “Mimi na huyo jamaa hatufanani kabisa yaani, sisi ni watu wawili tofauti. Wote tunaimba Bongo Flava, Wote tunafanya kitu kimoja lakini makoo tofauti sababu koo la Diamond sio koo langu mimi tuko tofauti kabisa.”
Muimbaji huyo aliongeza kuwa hana urafiki wowote na Diamond licha ya kwamba wakikutana husalimiana.
“Mimi nachoamini sina ushkaji naye, sio lazima kuwa na ushkaji naye lakini ni mtu ambaye ananijua, namjua ‘hi mambo, vipi poa, salama’ hatuna matatizo yaani.”
Read more ...

Monday, October 14, 2013

Video: Diamond PlatnumZ Awatisha P Square Cheki hapa Ujionee Mwenyewe.

P-Square waanze kumuogopa Diamond Platnumz kwa kuwafundisha namna hit single yao, Temptation inavyotakiwa kuimbwa live? Kuna kila sababu, kwenye show yao ya mwezi ujao wakamtafuta Diamond ili awasaidie wakati wa kuimba huu?

Kuna kila uhalali kusema kuwa Diamond hajawahi kuimba vizuri live kama kwenye video hii ya kipindi cha Coke Studio Africa.
Akiimba pamoja na rapper wa Afrika Kusini, HHP na huku akisindikizwa na bendi moja hatari sana, Diamond ameonesha kuwa, muziki mzuri wa live si kitu wasanii wa Tanzania wa aina yake wanashindwa kuufanya kwa ustadi, kama tu kukiwa na sound na bendi inayojua kazi yake.
Read more ...

Wednesday, October 9, 2013

Aaah! KUMBE "Ndivyo ilivyo kati ya Wema na Diamond" Usisubiri kuambiwa Jionee mwenyewe!




Utata  umeendelea  kuibuka kuhusu picha zinazosadikiwa ni za hivi karibuni zikimwonesha Wema Sepetu na Nasib Abdul "Diamond Platnumz" katika nyakati tofauti kwenye nchi moja huko Asia wakiwa  kimahaba  CHUMBANI

Picha hizi zimehusishwa na usaliti wa Diamond kwa mpenziwewa sasa aitwaye Penny, na gazeti moja la udaku lilichapisha habari kuwa wawili hao hawapo katika hali  nzuri  baada ya Diamond kurudiana na aliyekuwa mpenzi wake, Wema.  

 Wakati Wema akiripotiwa kuwa alikuwa China kwa
ajili ya sherehe za kumbukumbu ya sikukuu yake ya kuzaliwa, Diamond aliripotiwa kipindi hicho hicho akiwa Malaysia kwa ajili ya shughuli zake za kutumbuiza na burudani.


  Baada  ya  picha  hizi  kuvuja,Diamond  amefunguka  na  kujitetea  kuwa  eti  walikuwa  wana shoot movie  yao  mpya, lakini hembu tutumie macho kwa kufananisha hizi picha ili  tuupate  ukweli.


Angalia picha ya juu hair style ya Diamond na mawani aliyovaa. Picha ya juu alipiga Diamond akiwa dukani huko Malaysia na picha ya chini ni moja ya picha zilizovuja
Angalia tena picha ya juu hair style ya Wema pamoja na hand bag yake, then angalia picha ya chini hair style ya
Wema pamoja na begi lake. Picha ya juu ni moja kati ya zilizovuja na ya chini alipost Wema akiwa bara la Asia lakini ilisemaka yupo Hongkong




 
Angalia simu aliyotumia Wema kupiga hizi picha hapo chini na juu, picha ya chini nayo imevuja

 


Read more ...

Saturday, August 31, 2013

Picha: Pozi la Diamond na Linah lawa Gumzo, Penny apewa Tahadhari.


Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ amenaswa na msanii mwenzake, Esterlina Sanga ‘Linah’ wakiwa kwenye mapozi ya kimahaba ambayo yametafsiriwa vibaya.
 

Katika tukio hilo lililojiri juzikati kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora ndani ya Tamasha la Serengeti Fiesta, Diamond alishuhudiwa akiwa amempakata Linah ndani ya basi huku mikono ya jamaa huyo ikishika maeneo nyeti.
 
Mara baada ya kutimba uwanjani hapo wakitokea hotelini tayari kwa kufanya shoo, Diamond na Linah walibaki kwenye basi wakiwa wamepakatana na hata msichana huyo alipomaliza shoo yake kali mishale ya saa 3: 00 usiku, alirejea mikononi mwa Diamond ambaye alimpachika mapajani.


Kwa mujibu wa mashuhuda, kama kweli mchumba wa Diamond, Penniel Mungwilwa ‘Penny’ anakubali mambo kama hayo, basi atakuwa na roho ngumu au moyo wa chuma.
 
Siyo mara ya kwanza Diamond na Linah kuripotiwa wakiwa wamepozi kimahaba kwani mwaka jana walifanya hivyo wakiwa jijini Mbeya hivyo kutafsiriwa kuwa inaonekana ni katabia kao kabaya wanakaendekeza.
Read more ...

Friday, August 30, 2013

Mfululizo wa Picha ndani ya uzinduzi wa Video mpya ya Diamond Platnum. Diamod Katisha

Hamis Mwinjuna A.k.a Mwana F.A alikuwepo pia kushow Love....

Interiew zinahusika sana sehemu kama hizi....


Sauda wa Bongo Beats ya Star Tv nae akukosekana ndani ya nyumba.....
Chege Chigunda Toka TMK nae alikuwepo.....
Flowers awakosekanagi sehemu kama hizi.......
wakiongozwa na Number One Diva Hamisa
hassani Mobeto.


Mzee Muhidini Gurumo nae akukosekana
ndani ya Nyumba.....Furaha Ilioje kumuona
Nguli wa Muziki wa Dansi nchini akiudhuria
kwenye kitu chako,binafsi nimefurahi
sana uwepo wake ulizidi kuimarisha moyo wangu.

Prince Brother Man Dully Sykes akiwasili
ndani ya Nyumba pembeni na FloweR
Shadee toka Clouds Tv,presenter wa Cloud 9...



Shadee & Dully...Mmmmmh....??? Aya sina usemi
Kama kawaida......
Sarah A.k.a Shaa nae ndani 
Movement zikiendelea na mahojiano mbalimbali
kati ya wasanii na presenters wa vituo mbalimbali
vya Habari & Blogs kiujumla wakiwa kazini....






Mama yangu Mdogo yanii nikimaanisha Mdogo
 wake na mama yangu mzazi Bi Sandrah Sammy
Asha Baraka,Manager na Owner wa Twanga Pepeta nae alikuwepo...





Mwenyewe Naseeb Abdul Nilipowasili,Shuguli ikawa imefikia patamu sasa......






Nikijibu maswali tofauti tofauti toka kwa waandishi wa Habari...


Jacquline Wolper toka Bongo Move nae akukosekana.....



Jacquline wolper & Qboy Msafii......



Kwenye Red Carpet nikiwa na Dada yangu,Rafiki yangu wa karibu
Penniel Mungiwa,Presenter wa DTV...
Thanks For Coming Buddy.....
The True Boy Is in the building....
Proffesor Jay a.k.a Father House nae alikuwepo
 kushow Love kwa mdogo wake.....






Read more ...
Designed By ApexbnewZ