Top News
Showing posts with label Lulu. Show all posts
Showing posts with label Lulu. Show all posts

Friday, November 1, 2013

Lulu atoa msaada wa pesa kwa wagonjwa wa Saratani katika hospitali ya Ocean Road

Muigizaji wa filamu, Elizabeth Michael aka Lulu amewatembelea wagonjwa wa saratani waliolazwa kwenye hospitali ya Ocean Road jijini Dar es Salaam leo na kuwapa msaada wa pesa ili ziwasaide kwa matibabu na mahitaji mengine.
75a4dc9a42c411e3b01422000aaa05b1_8

Kupitia Instagram, Lulu aliwataka Watanzania wawe na utaratibu wa kuwasaidia wagonjwa wa aina hiyo kwa chochote walichonacho.

“Naamini mimi sio mwema sana mpaka Mungu akaniwezesha kuona mwezi huu nikiwa mzima na mwenye afya. kwa kutambua hilo nimeanza mwezi huu kwa kupita katika hospitali ya Ocean Road na kutoa mchango ili kuwasaidia wagonjwa wa CANCER na tuwe na utaratibu wa kuwakumbuka wahitaji kwa chochote tulichonacho,” aliandika.
Read more ...

Friday, October 11, 2013

Tatoo ya Aliyoichora Lulu yabeba Ujumbe mzito Ukibahatika kuisoma lazima uwe na Maswali Tele.


Tarehe 9/10 kabla hajalala mwigizaji Lulu aliwaonyesha mashabiki zake picha ya tatoo yake mpya ambayo imechorwa juu ya kifua karibu na bega ikiwa ni picha aliyoipost na ikaambatana na maneno yafuatayo.

“Kumekuwa na kawaida ya watu kuongea na kuhukumu wenzao bila ya kujua wanachokiongelea pengine!! kwa upeo wangu mdogo nafahamu sisi wote ni binadamu na tunamtegemea mtu mmoja MWENYEZI MUNGU…lakini cha kushangaza kuwa watu wako busy kuhukumu wenzao kuliko hata huyo mwenye cheo chake, hivi Mungu angetaka kufanya kama wanadamu tunavyofanya tungeangaliana kweli? nadhani umefika wakati wa kumuachia mwenye majukumu yake kufanya kazi…tuache kujipa u busy usio wa lazma….!!!ONLY GOD CAN JUDGE ME….Gud nyt fam”


Read more ...

Thursday, September 12, 2013

Foolish Age ya LULU yamuweka roho juu sasa asakwa.

KUFANIKIWA kwa uzinduzi wa filamu ya Foolish Age ya msanii Elizabeth Michael ‘Lulu’ uliofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam, kumemfanya kinda huyo anayetingisha katika tasnia hiyo kupata vitisho kutoka kwa mastaa wenzake.
Habari kutoka vyanzo mbalimbali ndani ya fani hiyo zinasema katika uzinduzi huo, msanii huyo alifunika na kuonyesha dalili zote za kuwazima mastaa wenzake ambao kwa muda mrefu wamekuwa juu.
Taarifa hizo zinasema staa huyo wa Bongo Muvi anatafutwa kwa kila namna, usiku na mchana ili kuhakikisha nyota yake inafifia.
Madai hayo yamekuja zaidi baada ya uzinduzi huo kufana kwani pamoja na mambo mengine, hata jinsi alivyokuwa amejipanga kwa walinzi wake, lilikuwa ni jambo kubwa ambalo linafanana na inavyotokea katika shughuli za mastaa mbalimbali wa majuu.
Mwandishi wa gazeti hili aliamua kufunga safari hadi maskani kwao pande za Tegeta, lakini msanii huyo hakupenda paparazi afike kwao hivyo mazungumzo yao kufanyika kama ifuatavyo kwa njia ya simu ya kiganjani.
Mwandishi: Mambo vipi Lulu?
Lulu: Salama tuu za kwako?
Mwandishi: Salama, vipi umesikia vitisho vyako kutoka kwa mastaa wa Bongo Muvi wanaodai kuwa umekuja kuwapita kisanii?
Lulu: Hapana sijasiki, lakini kama wanatoa vitisho lazima wakubaliane na ukweli kwamba lazima awepo wa kwanza na wa mwisho, wakaze buti.
Mwandishi: Umejipangaje kukabiliana na hilo?
Lulu: Najipanga kufanya kazi mimi kama mimi na wao wafanye kama wao, wakijifanya kuwa kama mimi haiwezi kuwa hivyo, mbona mastaa wa ughaibuni kama Beyonce na Rihanna wako tofauti? Lazima awepo wa kwanza mpaka wa 10 hatuwezi kulingana.
Mwandishi: Kuna lolote la kuongeza juu ya hilo ama wito kwa wasanii?
Lulu: Wajipange kufanya kazi kwa nguvu zote, wasifanye kama mimi wafanye kama wao,
Mwandishi: Asante Lulu nakutakia siku njema
Lulu: Ok, sawa kazi njema
SOURCE: GPL
Read more ...

Saturday, August 31, 2013

Picha: Uzinduzi wa "Foolish Age" ya Lulu yawa Kufuru mapedeshe wamwaga mihela

UIMBAJI stadi wa Wibo wa YAHAYA wa Nguli wa muziki wa Kizaki kipya Lady Jay Dee umemjaza mahela Msanii wa Filamu aliyejizolea umaarufu kwa miaka ya hivi karibuni, Elizabeth Michael ‘Lulu’ wakati akiimba wimbo huo na Jide wakati wa uzinduzi wa Video yake mpya na yakwanza kusimama peke yake ya FOOLISH AGE.

 

 
 
 
 
 
MSANII wa Filamu Bongo, Elizabeth Michael 'Lulu', usiku wa kuamkia leo amefanikisha zoezi la uzinduzi wa filamu yake mpya inayokwenda kwa jina la Foolish Age .

 Baada ya move hiyo kali ya dakika 120 iliyooesha ukali wa staa huyo kuoneshwa kwa dakika 20 tu na kubakisha zingine 100 kusubiri wateja kuziona majumbani kwao alipanda jukwaani kujitambulisha na kutoa shukrani kwa wamepenzi wa tasnia ya filamu nchini Tanzania kwa muitikio wao alipanda na kuimba wimbo huo wa Yahaya.
Akianzia kuimba kiitikio cha wimbo huo akiwa Back Stage, Lulu aliwashangaza watu pale alipomudu vyema wimbo huo kiasi cha mashabiki ‘Mapedeshee’ wakiongozwa na Pedeshee Rich Rich, kupanda jukwaani na kumtunza fedha kibao ambazo hakika zilimpagawisha msanii huyo na mwisho wa wimbo huo alisema mziki unalipa.
Tukio la uzinduzi huo lilifanyika katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar, na kuhudhuriwa na mastaa kibao wa tasnia mbalimbali hapa Bongo, wakiwemo; Judith Wambura 'Lady Jaydee', ambaye alitumbuiza sambamba na Barnaba na Amini.

 Wasanii mbalimbali walihudhuria show hiyo usiku huu pale Mlimani City




 Lulu akizungumza machache mara baada ya Move yake hiyo kuoneshwa kwa mashabiki na wapenzi wa filamu Tanzania ndani ya Ukumbi wa Mlimani City.



 Wadau walifuatilia burudani...

 Jide akikamua jukwaani...

 Mama na mwanao ni kama chanda na Pete... huyo ni Natasha (kulia) na Bintiye Monalisa.

 .... Walitunzana tu kivyao vyao...

 noti alizo tuzwa
 Rich Rich akimwaga noti


 Wadau wakifuatilia uzinduzi huo wa Filamu.

 Furaha ilitawala

 Mwogozaji wa Filamu za Kibongo, Leah Mwendamseke nae alikuwepo kuangalia kazi hiyo ya Lulu.

 Waongoza Shughuli hiyo watangazaji wa Redio na TV Double G na mwana dada kutoka Times FM walikuwepo.



Baada ya move hiyo kali ya dakika 120 iliyooesha ukali wa staa huyo kuoneshwa kwa dakika 20 tu na kubakisha zingine 100 kusubiri wateja kuziona majumbani kwao alipanda jukwaani kujitambulisha na kutoa shukrani kwa wamepenzi wa tasnia ya filamu nchini Tanzania kwa muitikio wao alipanda na kuimba wimbo huo wa Yahaya.

Akianzia kuimba kiitikio cha wimbo huo akiwa Back Stage, Lulu aliwashangaza watu pale alipomudu vyema wimbo huo kiasi cha mashabiki ‘Mapedeshee’ wakiongozwa na Pedeshee Rich Rich, kupanda jukwaani na kumtunza fedha kibao ambazo hakika zilimpagawisha msanii huyo na mwisho wa wimbo huo alisema mziki unalipa.

“Jamanieee kumbe mziki unalipa ile mbaya yaani  nimeimba ubeti mmoja tu hapa ona hela kibao, kuanzia sasa na mimi nitaanza kuimba mziki”, alisikika Lulu akisenma huku akishangiliwa na mashabiki wake.
 
Read more ...

Monday, August 26, 2013

Baada Ya Foolish Age ya Lulu Kupigwa stop sasa yaachiwa

 
Bodi  ya   ukaguzi  wa  filamu  Tanzania  imeridhia  na  kuiruhusu  filamu  ya  Foolish Age  ya  Lulu  Michael  iingie  sokoni  baada  ya  kuizuia  hapo  juzi....

Filam  hiyo  ilizuiliwa   kutokana  na  mavazi  ya  nusu  uchi  yaliyokuwa  yamevaliwa  na  washiriki  wake  na  kumtaka  Lulu  Michael  aifanyie  marekebisho  kwa  kuviondoa  vipande  hivyo  ambavyo  vilikuwa  kinyume  na  maadili  ya  kitanzani....

Filamu hiyo  ambayo yupo Lulu, Diana Kimaro, Jengua na Hashim Kambi itazinduliwa tarehe 30 mwezi huu katika ukumbi wa Mlimani City

Kupitia  account  yake  ya  instagram, Lulu  amepost  ujumbe  huu.

 
Read more ...

Friday, August 23, 2013

BODI YA UKAGUZI YAIPIGA STOP FILAMU YA FOOLISH AGE YA LULU.

Bodi ya ukaguzi wa filamu na michezo ya kuigiza nchini imeipiga stop filamu ya Foolish age ya msanii wa kike mwenye mvuto Bongo Elizabeth Michael ‘Lulu’ baada ya kukuta picha zilizo nje ya maadili ya Kitanzania katika filamu hiyo, filamu hiyo ambayo ilipanga kuzinduliwa mwezi huu tarehe 30 katika ukumbi wa Mlimani City inahitaji marekebisho.

Kikwazo kilichoikumba filamu hiyo ni nguo fupi zilizotumika katika waigizaji walioshiriki katika filamu hiyo ambayo inatabiriwa kufanya vizuri katika soko la filamu Bongo kama itafanikiwa kuzinduliwa na kuingia sokoni, juhudi zinafanyika kuhakikisha kuwa marekebisho yanafanyika ili kwenda na ratiba kama ilivyopangwa.

Hivi sasa baada ya urasimishaji wa filamu mamlaka na taasisi zinazohusika na masuala ya filamu zimekuwa makini na kuhakikisha kuwa filamu zinazoingia sokoni na zile zinazozinduliwa kukaguliwa kabla ya kufanyika kwa matukio hayo kama ilivyokuwa awali, kama filamu hiyo ya Foolish age itashindwa vigezo vya madaraja yanayotolewa na Bodi hiyo haitaonyeshwa.
Read more ...

Friday, August 16, 2013

Lulu kuizindua filamu yake mpya ‘Foolish Age’ August 30

Muigizaji wa filamu nchini, Elizabeth Michael aka Lulu anatarajia kuvunja ukimya wake kwenye big screen kwa kufanya uzinduzi mkubwa wa filamu yake mpya ‘Foolish Age’ tarehe 30 mwezi huu kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
BPioqRICEAAvPGK
Uzinduzi huo utasindikizwa na burudani kutoka kwa Lady Jaydee na Machozi Band.
“Hatimaye narudi kazini, nahitaji support ya mashabiki wote wa Lulu na mashabiki wa Bongo Movie,” anasema Lulu.

Kiingilio kwenye uzinduzi huo kinatarajia kuwa shilingi 30,000.
Read more ...

Monday, August 12, 2013

Lulu adondosha Ujumbe Mzito kwa Watanzani.!

Jana kupitia mtandao, mwanadada Elizabeth Michael (Lulu) aliandika ujumbe huu kwa watu wote watakaopenda kuusoma na kuufanyia kazi katika maisha yao. Ujumbe huu ni ujumbe wa upendo na sio vibaya ukitafakari na kuufanyia kazi.
Mwanadada Lulu aliandika…
“Umeshawahi kujiuliza umempa nini Mungu?una afya na una Uwezo wa kufanya chochote japo Kuwa unamkosea na kutenda dhambi kila Leo?unajua ni wangapi walitamani kuiona siku ya Leo lakn hawakuweza!?unajua wapo walioweza kuiona lakini wanapita katika majaribu magumu sana!?je unahisi wewe unafaa sana?au ni msafi sana!?au ni mzuri sana!?laah hashaaa....sio kwa Uwezo wako ni kwa NEEMA YA MUNGU TU”
Tafakari!
Read more ...

Tuesday, July 30, 2013

Thursday, July 18, 2013

KWA HILI ELIZABETH MICHAEL (LULU) TUMUELEWEJE..

Wengi tunavo fahamu Lulu sio Mwislam Ila pia si vibaya yeye kuungana na waslam kuadhimisha mwezi huu mtukufu kama imani zao zinavyo ruhusu. Ila swali langu limekuja kutokana na Ninavyo mfahamu mwana dada huyu... ni kweli huu muonekano wake wa nje kaudhamiria au kafuata tu mkumbo by da way sipaswi kumsemea loote kwani yeye ndio anae ufamu ukweli na anachokimaanisha.
Read more ...
Designed By ApexbnewZ