Top News
Showing posts with label Ney Wa Mitego. Show all posts
Showing posts with label Ney Wa Mitego. Show all posts

Wednesday, October 16, 2013

Ujumbe Aliouandika Ney Wamitego Instagram Unatisha.


Mpaka sasa ney haja sema ni nani na nini kimepelekea yeye kuandika hivi kuhusu maisha yake ya muziki. Ila inaonyesha hapa kati amekutana na misuko suko kwenye ,mishe zake, kuchukiwa na kutokukubalika kunaweza pelekea mtu kusema yote haya.
Bonyeza Read More Kuona Ujumbe Huo

Read more ...

Monday, August 12, 2013

Yamemkuta Ney Wa Mitego Sasa Apokea Vitisho kwa watu aliowatuhumu kuchakachua hela za msiba wa Ngwea

Msanii wa Hip Hop, Nay Wa Mitego amesema haogopi vitisho anavyoendelea kupata baada ya watu aliowatuhumu kwenye wimbo wa mpya, Salam Zao’ kuwa walichukua pesa za rambirambi za msiba wa marehemu Albert Mangwair.
1173664_401068240004866_1674635065_n
Kupitia akaunti zake za Facebook na Instagram, Nay ameanza kuandika na kufichua vitisho anavyopokea na huku akiwataka waliochukua pesa za marehemu Ngwair wazirudishe kimya kimya.
“Zipo nyingi zingine za vitisho,nitazipost zote watu wangu mujue leo nimeanza na iyo..!! Ukweli unauma sana!! siogopi vitisho vyenu,, pelekeni hela kwa ndugu wa marehem bado nafasi mnayo ata kimya kimya,, mi Nikifa sihitaji kamati za ki**enge kwenye msiba wangu, maana watu wanafanya misiba yetu mitaji yao,” ameandika Nay.
Read more ...

Sunday, August 11, 2013

Kwa Ujumbe huu unaashiria Ney Wa Mitego Na Sweety wake Mambo Sii shwari


Hatujathibitisha bado lakini tunahisi kuna ‘Tatizo’. Kupitia account yake ya Instagram Nay wa Mitego amekuwa akiandika ujumbe wenye mafumbo baada ya kuusoma ndani ya mistari (read between the line) tumegundua huenda mambo si mazuri kati yake na mpenzi wake ambaye hivi karibuni alikuwa akitarajia kumzalia mtoto lakini mimba ikaharibika.

Nay ambaye jina lake halisi ni Emmanuel Munisi, ameanza kwa kuandika ujumbe huu: Sasa mapenzi basi# by diamond Platnumz..!! Single boy# Ally Kiba#966’

Baada ya muda kidogo ameandika tena:

Niko ivi,,, nikikupenda nakupenda kwa asilimia 100# na kila m2 atajua juu ya upendo wangu kwako..!! Bt ukizingua nakuacha na ninakusahau kwa asilimia 200# na kwa muda mchache 2. Nikiamua huwa sirudi nyuma..!!# Mwanamke mjinga ataivunja ndoa yake kwa mikono yake ye mwenyewe# by Linex.#966’

Tunahisi mambo si mazuri kwenye ulimwengu wa mapenzi wa Nay, Itafahamika.


Read more ...

Friday, August 2, 2013

Ney Wamitegeo Amva Zitto Kabwe na Madam Rita ...

Mfalme wa kudiss Tanzania, Nay wa Mitego amerejea tena kuchafua hali ya hewa kwa kutengeneza mijadala kwenye radio na kwenye mtandao kwa ngoma yake mpya, Salam Zao.

Kwenye Salam Zao, Nay ameendeela kufanya kile akifanyacho kwa uzuri (do what he does best) kuponda.
 
Awamu hii list ya aliowadiss imeongezeka zaidi na kuingia pia kwenye siasa huku akiendelea kuwapa madongo wana hip hop wenzie.

Ameanza kwa kumdiss Madee kwa kusema kuwa yeye ndio rais wa Manzese na kwamba Madee amesanda. “Mi ndo rais wa Manzese yule tozi kasanda, Manzese mikono juu naiongoza kamanda,” anachana Nay.

Nay wa Mitego ameendelea kuwadiss wana hip hip huku akiijita kuwa yeye ndio gangster rapper na anatengeneza hela huku wengine wakinuka vikwapa. Hakusita pia kuwarushia bombshell Weusi. “Yo Mchomvu wape salam ‘Kubumkubum’ waimbie watakufa njaa muziki umebadilika,” anarap Nay.

Nay pia amemdiss Zitto Kabwe kwa kurap:
 
 “Word up Diamond, mwanangu wewe si mtoto wa Kigoma, mpe salama Zitto Kabwe mwambie afanye siasa aachane na Bongo Flava huku hatumtaki kabisa, maneno mengi, propaganda hajui kutekeleza, Kigoma Allstars tayari kawatelekeza.”

Rapper huyo pia amerap kuwa wapo watu waliojipatia utajiri kutokana na misiba ya Mangwea na Kanumba.

“Wanamiliki gari, wameota na vitambi kwa hela za rambirambi, mkizingua nawataja,”anasisitiza. Anasema tangu kifo cha Kanumba Bongo Movies imekufa na haiuzi tena.

Pia hajamuacha mwanzilishi wa shindano la Bongo Star Search Rita Paulsen kwa kudai kuwa licha ya kuwapa zawadi kubwa washindi, wameendelea kupigika mtaani.

“Hizi Salam ziende kwa madam Rita na Bongo Star Search. Mshindi analipwa nini mbona kama magumashi?! Namuona Walter Chilambo kapigika kama zamani, Haji Ramadhani kachoka yupo kitaani. Nauliza milioni hamsini zao anazila nani, acheni ubabaishaji wekeni mambo hadharani.”

Isikilize Hapa

Read more ...
Designed By ApexbnewZ