Top News
Showing posts with label Wastara Juma. Show all posts
Showing posts with label Wastara Juma. Show all posts

Monday, August 12, 2013

Hivyo ndivyo mwanadada Wastara alivyosherehekea sikukuu ya Eid.






    • Mwanadada Wastara aliamua kusherehekea sikukuu ya Eid kwa kuamua kwenda kutembelea kaburi la mumewe Marehemu Juma Kilowoko (Sajuki) kwenye makaburi ya kisutu jijini Dar es salaam
      Tukio hili lilitokea siku ya ijumaa iliyopita , siku ya Eid mosi ambapo mwanadada huyo alionekana katika picha mbalimbali akifanya usafi kaburini hapo.
      “Sikukuu yangu nimeitendea haki sana kwa kwenda kuzuru kaburi la mume wangu, alhamdullilah nimefarijika sana, kimwili siko naye ila atabaki kuwa fikrani mwangu…Alisema Wastara.
      Read more ...

      Thursday, August 8, 2013

      "Kumbe Wasara Aliwahi Kuolewa Kabla yakua na Sajuki" Mume huyo Aaza Kimbembe.


      MIEZI nane baada ya kufariki dunia mumewe Juma Kilowoko ‘Sajuki’, hatimaye mume wa pili wa staa wa filamu za Kibongo, Wastara Juma aitwaye Ahmed Kushi ameibuka na kudai kwamba anatambua kwamba staa huyo bado ni mkewe na anat aka ampatie mwanaye aliyezaa naye.
      Kwa muda mrefu kulikuwa na taarifa kuwa Wastara aliachana na mwanaume huyo kwa talaka kabla ya kuolewa na Sajuki lakini kuibuka kwake na madai kuwa bado mwanadada huyo ni mkewe kumezua mshangao mkubwa.
      Akizungumza hivi karibuni,Kushi alifunguka kwa mara ya kwanza kuwa yeye na Wastara walifunga ndoa ya Kiislamu mwaka 2000 na kujaliwa kupata mtoto mmoja wa kiume aitwaye Fares.
      Alisema: “Kisheria bado ni mke wangu kwa kuwa nilikuwa nimempa talaka moja tu wala hazikufika tatu,” alisema Kushi na kudai kwamba ndoa yake na staa huyo ilidumu kwa mwaka mmoja na nusu na kuvunjika kutokana na kutawaliwa na migororo.
      Jamaa huyo alidai kuwa zaidi ya mara tatu amekuwa akimtaka Wastara ampatie mwanaye huyo ambaye kwa sasa ametimiza miaka minane bila ya mafanikio.
      Kushi alipobanwa na kumuulizwa kwa nini ameibuka wakati huu baada ya Sajuki kufa na mbona hakujitokeza kwa zaidi ya kipindi cha miaka kumi iliyopita? Pia akaulizwa kwa nini ameamua kutafuta umaarufu kwa kumdhalilisha? Akaishia kukaa kimya.
      Baada ya Kushi kuibuka na ishu hiyo yenye utata, gazeti hili lilizungumza na Wastara ambapo alikuwa na haya ya kusema:
      “Kuhusu mtoto, kama kweli alikuwa na lengo la kumchukua mwanaye na ananijua, basi atakuwa anawajua wazazi wangu hivyo angefuata utaratibu.
      “Hakuna utaratibu kama huo kama kweli anamhitaji mwanaye angeenda kwa wazazi wangu, huko ni kunidhalilisha kwa kuwa ananiona mnyonge baada ya kufiwa na mume wangu Sajuki.
      “Kama siyo kunidhalilisha ni nini? Naomba asitumie jina langu kutafuta umaarufu kwa kunichafua. Naomba aache kwa sababu ananiongezea maumivu juu ya maumivu.”
      Kuhusu madai kwamba bado ni mkewe, Wastara alilia: “Hivi huyo mtu alikuwa wapi muda wote nikiwa na Sajuki? Mbona hakuibuka wakati mume wangu akiwa hai? Najua anatumia kigezo cha kuondoka Sajuki kunionea lakini Mungu anajua.”
      Pamoja na kumbembeleza aeleze kama kweli aliwahi kufunga ndoa na Kushi, Wastara alisema: “Sitaki kumzungumzia mtu, naomba watu wawe na huruma kwangu, wasitumie kigezo cha kumpoteza Sajuki kunidhalilisha.”
      Alitafutwa shehe wa Msikiti wa Nuur wa Magomeni-Mapipa jijini Dar, Juma Simba ili kupata ufafanuzi juu ya talaka moja ambapo alimpinga Kushi kwa kusema kuwa kisheria Wastara si mkewe tena.
      “Kumpa talaka moja si sababu ya kuendelea kuwa mke wake mpaka leo hii, sheria inasema kuwa Kushi alitakiwa kumrejea Wastara kabla ya miezi mitatu kupita tangu alipompa talaka moja,” alisema na kusisitiza kuwa ndoa hiyo ilishakufa.
      Awali ilidaiwa kuwa Wastara aliwahi kuolewa mara mbili kabla ya kufunga ndoa na staa mwenzake wa filamu, Sajuki.
      Ndoa ya kwanza ya Wastara aliifunga mwaka 1998 na Juma Mpemba ambaye alibahatika kupata naye mtoto mmoja wa kiume aitwaye Samir.
      Sajuki alikuwa mume wa tatu kwa Wastara ambaye naye alibahatika kupata mtoto mmoja wa kike aitwaye Farheen.
      via-GPL
      Read more ...

      Saturday, July 20, 2013

      "WANAUME WALIO MSAIDIA SAJUKI WAMENIGEUKIA NA KUNITAKA KIMAPENZI"-WASTARA JUMA


      Wastara Juma amefunguka kuwa wanaume wengi waliokuwa wakimsaidia wakati mumewe Juma Kilowoko ‘Sajuki’ akiwa mgonjwa wanamgeuka na sasa wanamtaka kimapenzi.

      Akizungumza kupitia Kipindi cha Take-One katika Runinga ya Clouds chini ya Zamaradi Mketema, Wastara alisema baadhi ya watu ambao walikuwa karibu naye wakati Sajuki anaumwa sasa hivi wamegeuka na kumtaka kimapenzi, jambo ambalo linamuumiza na kumshangaza mno.

      Bishosti huyo alisema kuwa tofauti na wanaume hao ambao walikuwa wakimpa sapoti kipindi hicho, bado wapo wengine kibao kutoka nje na ndani ya nchi ambao wanatuma maombi kwake lakini anawaona wote ni matapeli na wanamtamani tu hivyo hayupo tayari kuingia kwenye uhusiano wa aina hiyo.

      “Kweli ninaumia sana kwa sababu ninakaa na kujiuliza hawa wanaume walikuwa wanasubiri mume wangu afariki dunia ndiyo wanitongoze?

      “Kusema kweli inanishangaza, hata watu ambao sikuwadhania kabisa eti nao wananitaka, watu wajue kwa sasa sipo tayari kuwa na mwanaume.

      “Sitaki kukurupuka kwa sababu naweza nikaingia kwenye shimo la taka kwani jamii itanikimbia kutokana na kunuka, natamani kumpata mwanaume anayefanana na mume wangu kitabia.

      “Uvumilivu wangu na uzuri ulitokana na kutunzwa siyo aje mtu anayetaka nikavumilie shida, hilo sitaki litokee, namuomba Mungu sana,” alisema Wastara.
      Read more ...

      Xclusive:Picha Wastara Juma Aaza kuphotoa Move yake mpya...!



      Hatimaye mwadadada Wastara Sajuki amerejea tena kwenye ulimwengu wa filamu baada ya kuwa kimya kwa muda mrefu kwenye tasnia hii kutokana na matatizo aliyoyapata ya kuondokewa na mumewe Juma Kilowoko (Sajuki) mnamo mwezi wa January mwaka huu.



      Akizungumza katika utengenezaji wa Filamu yake mpya ya kwanza atakayoiachia wastara amesema Filamu hii mpya wastara amesema kuwa itahusu maisha ya kawaida ya mwanadamu na jinsi ambavyo matatizo yanayomkabili binadamu yanavyoweza na kumuathiri kisaikolojia na kumpelekea kufanya mambo ambayo hakuwai kuyafikiria.

      Wastara amesema kisa kikuu kwenye filamu hii yake mpya ni jinsi familia moja iliyokuwa na maisha mazuri na baadaye mama wa familia kupata kansa ya kizazi na kupelekea kuondelewa kizazi chake kabla ya kufiwa na mtoto wake pekee aliyekuwa naye na namna ambayo mumewe anavyojaribu kumliwaza mkewe kwa matatizo hayo yanayotokea.



      Wastara amesema kuwa kwenye Filamu hii ameshirikia na waigizaji Yusuph Mlela na Nisha pamoja na mwigizaji mweingine aliyemtaja kwa jina la Hamida na amewataka wapenzi wake wote wakae mkao wa kula kwa ajili ya Filamu hii inayotarajiwa kutoka mwezi wa tisa.






      Credit:bongomovies
      Read more ...

      Thursday, July 18, 2013

      WASTARA JUMA: NAHITAJI MUME ILA..........!

       
      STAA wa filamu za Kibongo, Wastara Juma amesema hana haraka ya kuolewa kwani anahitaji mume na si mwanaume  wa kupita

      Akizungumza na mwandishi wetu hivi karibuni, Wastara alisema kwa sasa yupo huru kutoka na mtu yeyote ampendaye kutokana na sheria na dini inavyosema ila kwa sasa shughuli za kuigiza zimembana.

      ‘Nahitaji mume na si mwanaume  wa kupita,  awe mvumilivu, mchapakazi pia awe na hofu ya Mungu. Kwa sasa nafanya filamu zangu kama kumuenzi marehemu mume wangu,” alisema Wastara.
      Read more ...
      Designed By ApexbnewZ