Top News

Sunday, March 24, 2013

Lulu / Elizabeth Michael: HIVI NDIVYO TULIKUA TUKIMKUZA KALE

Si muda mrefu tangu Elizabeth Michael maarufu kama Lulu kupata dhamana na kurudi uraiani baada ya kusota rumande kwa takribani kama miezi nane hivi, alikokua ameshikiliwa kwa kosa la kuuwa bila kukusudia msanii mwenzake Marehemu Steven Kanumba.
Lulu alirudi uraiani kwa furaha na wasani wenzake pamoja na mashabiki wanaopenda kazi zake za sanaa walimpokea kwa Furaha sana. Ila umefika wakati jamii inayomzunguka kutazama aina ya maisha ambayo tulikua tukimkuza nayo, kama wanahabari, kama taifa na kama mtu mmoja mmoja.
Je, haya yalikuwa yanashamiri kwasababu alikuwa akiyalazimisha yeye mwenyewe au kwakuwa yalikuwa yakifanyika sisi tunashabikia kwa kuwa waandikaji, wasomaji na hata wanunuaji wazuri wa habari za skendo zenye kumhusu
Tulimruhusu, kwa ridhaa yetu wenyewe kufanya mambo kama haya, huku tukiyashabikia ama kwa kutoa maoni yenye kuonyesha amependeza kwa mikao ya namna hii nk. Ni nani alikemea hali hizi hadharani? Ufike wakati tuonye, tuelimishe kama kweli tunampenda na hatuko tayari kuona yanayo mpata ni mabaya zaidi.

Hata alipozungumza jambo ambalo halikuwa na mantiki, tulilipa uzito mkubwa sana, kuliko hata aliyelizungumza. Hatukujali ulikuwa ujinga, upumbavu, au nini. Hatukujali kuwa tunazidi kumpotosha zaidi, tulijali kumjua kwa kila hali na tukamsukuma naye kuwa anafanya kila lililokuja mbele yake, bila kufikiri maana tuliokuwa tunayapokea yenye kumhusu hatukuwa tunafikiria pia.
Mwisho wa siku, akaona kwakuwa watu wanataka kumjua kwa namna yoyote ile, basi bora auze utu wake kabisa? Na tulivyo waungwana sana, wapo wenzetu ambao walijitokeza na kumpandia dau.
Naam, huyu ndio binti yetu Elizabeth Michael, maarufu kwa jina la Lulu, ambaye hivi sasa sisi ambao tumempa makuzi ya namna hiyo hapo juu, ndio sisi tuliofika wakati tukamshutumu na kumuna mkosaji asiye staili bila kujua mototo umleavyo ndivyo akuavyo. Umefika wakati tukatizma upya wapi alipotoka nani wapi anapokwenda na je tutamsaidia vipi kwa makuzi ya sasa ua tutaendelea nayale yale. Na hiyo ni sehemu ndogo mno ya malezi tuliyokuwa tukimpatia

Ninawaza kwa maandishi tu, na mawazo yangu yanaweza kuwa sawa na ya mwingine mwenye kuwaza sawa na mimi au tofauti na mtu anayewaza kinyume na mimi.




No comments :

Post a Comment

Designed By ApexbnewZ