Umepita
mwaka sasa toka marehemu Steven Kanumba afariki Dunia 07.04.2012
kutokana na ugomvi uliotokea kati yake na mpenzi wake, Elizabeth Michael
a.k.a Lulu. Katika kumkumbuka http://apexbnews.blogspot.com/ inakuletea historia yake fupi iliyoandaliwa na mtandao wa Bongo Movies.
Alikuwa
anajulikana zaidi kama “The great” kama mwenyewe alivyopenda kujiita.
Jina lake halisi ni Steven Kanumba. Alikuwa mmoja wa waigizaji wakubwa
sana ndani ya tasnia ya Bongo Movies.
Na
Katika historia ya tasnia ya filamu nchini Tanzania, Kanumba ndiye
aliyekuwa msanii wa kwanza nchini kufanya kazi nje ya nchi na kuweza
kuwavuta wageni kutoka nchi mbalimbali kuja kuigiza Tanzania, hasa
Wanigeria kama vile Mercy Johnson, Emmanuel France, Nkiru Silvanus,
Ramsey Nouah, na wengine wengi. Kanumba pia ameweza kuwaleta waongozaji
filamu kadhaa was Kinigeria nchini.
Moja
ya filamu zilizompa umaarufu sana kimataifa ni pamoja na Devil’s kingdom
nyingine kama Dar 2 Lagos na Cross my sin. Alikuwa mmoja wasanii wenye
uwezo mkubwa kifenda na utajiri wako ulikuwa unakadiriwa kuwa zaidi ya
shillingi milioni 300 za kitanzania.
Early life:
Steven
Kanumba alizaliwa tarehe 8 mwezi wa Kwanza mwaka 1984 huko shinyanga.
Kwa kabila alikuwa ni msukuma. Alipata elimu yake ya awali katika shule
ya msingi msingi ya Bugoyi, na kuendela na masomo ya sekondari huko
Mwadui huko huko shinyanga na baadaye kuhamia katika shule ya sekondari
ya Dar es salaam Christian Seminary akiwa kidato cha pili ambako alisoma
mpaka kidato cha nne na akaendelea na masomo ya kidato cha tano na sita
katika shule ya sekondari ya jitegemee iliyopo Dar es salaam.
Career:
Kanumba
alianza kuigiza toka alipokuwa shule ya msingi kabla ya kujiunga na
kikundi cha kaole sanaa group miaka ya tisini. Akiwa kaole kanumba
alikutana na walimu wa sanaa toka chuo cha sanaa bagamoyo na vyuo
vingine ambako alipata mafunzo zaidi ya uigizaji na baadae alikutana na
Dr. Nyoni toka Chuo kikuu cha Dar es Salaam ambako alweza pata mafunzo
ya uigizaji kwa muda wa miezi mitatu.
Baada
ya hapo kanumba alianza rasmi kuigiza filamu na filamu moja ya filamu
zake za kwanza kuigiza zilikuwa sikitiko langu na Johari ambazo zilimpa
umaarufu zaidi na kumuwezesha kufanya kazi nyingine mbalimbali ndani na
nje ya nchi.
Steven
kanumba alikuwa mmoja wa wasanii wa kwanza Tanzania kuweza kutembelea
studi za filamu za Universal Studio pamoja na Warner bros zilizopo huko
nchini Marekani. Pia kanumba alikuwa mtunzi wa nyimbo na alikuwa na
uwezo wa kupiga vifaa vya muziki kama kinanda na gitaa
Kifo:
Steven
Kanumba alifariki dunia tarehe saba (7) mwezi wa nne (4) mwaka 2012
baada ya kuanguka chumbani kwake kufuatia ugomvi baina yake na aliyekuwa
mpezi wake Elizabeth Michel (LULU).
Alifariki
muda mfupi baada ya kufikishwa Hospitali ya taifa ya Muhimbili. Mazishi
yake yalihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa nchi na umati unaokadiriwa
kufikia watu elfu thelathini (30,000).
Tutakukumbuka daima, Mungu akulaze mahala pema peponi, Steven Kanumba.
Ameen!!!
No comments :
Post a Comment