Baadhi ya kauli zilizotolewa na nyingi kuombewa mwongozo wa Spika ni kama ifuatavyo:
“Tutaliheshimu Bunge kama taasisi huru, lakini si
lilivyo sasa kama taasisi ya CCM,” Freeman Mbowe-Chadema, Kiongozi wa
Upinzani. “Sugu siongei na mbwa bali naongea na mwenye mbwa.” Juma
Nkamia-CCM.
“Ni wazi kuwa hata kauli ya Waziri Harrison
Mwakyembe imejaa utupu usio na matendo kwa kukataza wasafiri njiani
wasichimbe dawa.” Halima Mdee-Chadema.
“Kuna wabunge humu ambao wana mimba zisizotarajiwa bungeni.” Livingstone Lusinde-CCM.
“Ukiangalia kuna watu wanataka kuvuruga nchi
wakati wana watoto wachanga. Mimi mtoto wangu wa mwisho ana miaka
minane, halafu Slaa (Dk Willibrod Slaa) wa kwake sijui ana wiki ngapi.”
Livingstone Lusinde.
“Mbowe kaja hapa kajamba bungeni halafu kakimbilia kwenda kujamba Kibaha.” Mbunge wa Konde (CUF), Khatibu Said Haji Konde (CUF).
“Sikujua wabunge mnataka kuvuana nguo, hivyo nitatoa mwongozo wangu baadaye.” Job Ndugai, Naibu Spika.
Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Peter Msigwa
alisema, “Kuna tatizo la akili ndogo kutawala akili kubwa na hilo ni
tatizo la Serikali.”
“Serikali si sikivu na imevaa miwani ya mbao,” alisema Deo Filikunjombe-CCM.
“Wanapoongea watoto wa kiume, watoto watulie.” Mwigulu Nchemba-CCM.
“Hatupendi kusema ufanisi wake umepungua wala
kuendelea kubaki ofisini bila ya mkataba ni kutokana na kujipendekeza
kwa Rais na uhodari wake wa kukipendelea chama tawala na Serikali,
lakini tunapenda kusema wapo watu wenye sifa ya kuwa Msajili wa Vyama
vya Siasa.” Profesa Kulikoyela Kahigi.
No comments :
Post a Comment