- Atamani ushike kasi zaidi ya facebook na twitter
Mwanafunzi wa Chuo kikuuu cha Dodoma, ndugu Justice Donatus amefanikiwa kutengeneza mtandao wake wa kijamii uitwao MAYOCOO ambao utasaidia kuiunganisha jamii ya kitanzania na kimataifa..
Akiongea na mwandishi wetu mjini Dodoma, Justice ambaye ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu katika chuo hicho ameeleza furaha aliyo nayo kwa kutimiza ndoto yake ya muda mrefu ya kuja na mtandao mpya wa kizalendo ambao utaipiku mitandao ya kigeni kama Facebook na Twiitter
Mtandao huo ulizinduliwa rasmi Jumamosi ya wiki iliyopita chuoni hapo chini ya Usimamizi wa taasisi ya kuendeleza vipaji kwa vijana iitwayo AISEC na tukio hilo lilidhaminiwa na makampuni mbalimbali ikiwemo bank ya CRDB
Jiunge na mtandao huo hapo chini ili ufaidi matunda ya kitanzania
"www.mayocoo.com"
Juu na chini ni Wadau wa Mayocoo wakiwa katika picha ya pamoja baada ya uzinduzi huo
Justice Donatus akizindua mtandao huo
No comments :
Post a Comment