Top News

Monday, August 26, 2013

Fat Joe ajisalimisha mwenyewe jela kuanza kutumikia kifungo.

Rapper Fat Joe jana (August 26) alitweet ujumbe wa kuwaaga mashabiki wake kabla ya kwenda mwenyewe kuripoti jela ya Federal Detention Center, Miami , Marekani kuanza kutumikia kifungo cha miezi minne jela alichohukumiwa baada ya kukutwa na hatia ya kushindwa kulipa madeni ya kodi.

FAT-JOE (1)
Joseph Cartergena a.k.a Fat Joe alitweet, “FARE WELL MY PEOPLE IM BOUT TO TAKE THAT RIDE SEE U AT DIDDYS HOUSE FOR NEW YEARS#GODWILLINGINSHALLAH,”
Fat Joe hakuondoka hivi hivi bali aliamua kuwaachia mashabiki wake zawadi ya mixtape yake ‘The Darkside Vol. 3’ bure.
Fat Joe (June 24) alihukumiwa kifungo cha miezi 4 jela baada ya kushindwa kulipa madeni ya kodi (income taxes) zaidi ya $ 1 million kwa kipindi cha miaka miwili 2007 na 2008.
Kifungo hicho kinaambatana na faini ya $15,000 pamoja na usimamizi maalum wa mwaka mmoja baada ya kutoka jela.

No comments :

Post a Comment

Designed By ApexbnewZ