Jikubali ya Ben Pol ilikuwa ni video ya kwanza aliyoongoza Nisher kuchezwa Channel O, na sasa muongozaji huyo wa video kutoka Arusha, ameandika historia nyingine na video aliyomfanyia producer wa Transformax, Lucci Da Don.
Video hiyo imekuwa video ya kwanza ya Nisher kuwahi kukubalika na kuwekwa kwenye mtandao wa Marekani wa ViewHipHop.
“Nimefurahishwa na mapokezi ya video mpya ya #SUMU by #LUCCI… Kwa mara ya kwanza katika video zangu zote, video hii imefaulu kukubalika katika blog moja ya Marekani Kwa jina la “VIEWHIPHOP” yenye followers 43,336,” aliandika kwenye Facebook.
Video ya Lucci imewekwa kwenye video za wasanii ambao hawapo chini ya label yoyote (unsigned).
No comments :
Post a Comment