Wakuu wa idara ya Polisi nchini Kenya wamewaonya
waandisi wa habari kuhusu walivyoripoti matukio katika jumba la Westgate
ambako magaidi walishambulia zaidi ya wiki tatu zilizopita.
Onyo hili linakuja baada ya taarifa za wanajeshi
kufanya uporaji katika jengo hilo wakati wakipambana na magaidi hao
waliokuwa wamewateka nyara watu waliokuweme ndani ya jumba hilo.
Mkuu wa polisi, David Kimaiyo
alisema kuwa waandishi hawapaswi kutoa kuchochea Propaganda, au
kuwachochea wakenya wakati wakipeperusha matangazo yao.
Duru zinasema kuwa baadhi ya waandishi wa habari wamehojiwa na polisi hii leo.
Picha za CCTV zilizofichuliwa kwa waandishi wa
habari zilionyesha wanajeshi wakitoka ndani ya jumba hilo na mifuko ya
plastiki zilizoshukiwa kuwa na bidhaa kutoka katika mojawapo ya maduka
makubwa yaliyokuwa ndani ya jengo hilo la Nakumatt.
Hata hivyo jeshi limekanusha madai hayo na
kusema kuwa wanajeshi walikuwa wanachukua maji ya kunywa wakati wa
operesheni yao dhidi ya magaidi.
Takriban watu 67 walifariki ikiwemo wanajeshi na
mamia ya wengine kujeruhiwa kwenye shambulizi hilo liliosababishwa na
Al Shabaab kama walivyokiri. Waliwateka nyara watu ndani ya jingo hilo
kwa siku nne.
Pamoja na kupora, vyomo vya habari Kenya
vimesema kuwa baadhi ya wanajeshi waliuwana na wenzao wakati wa
operesheni yao kutoka na kile kilichosemekana kuwa ukosefu wa maelekezo
mazuri kuoka kwa wakuu wa usalama.
~BBC
No comments :
Post a Comment