P-Square waanze kumuogopa Diamond Platnumz kwa kuwafundisha namna hit single yao, Temptation inavyotakiwa kuimbwa live? Kuna kila sababu, kwenye show yao ya mwezi ujao wakamtafuta Diamond ili awasaidie wakati wa kuimba huu?
Kuna kila uhalali kusema kuwa Diamond hajawahi kuimba vizuri live kama kwenye video hii ya kipindi cha Coke Studio Africa.
Akiimba pamoja na rapper wa Afrika Kusini, HHP na huku akisindikizwa na bendi moja hatari sana, Diamond ameonesha kuwa, muziki mzuri wa live si kitu wasanii wa Tanzania wa aina yake wanashindwa kuufanya kwa ustadi, kama tu kukiwa na sound na bendi inayojua kazi yake.
Duh! Dimondo katishàaaaaa
ReplyDelete