Wednesday, April 02, 2025

Saturday, November 2, 2013

Lema aibua mazito ndani ya chadema ni kuhusu WASALITI na WANAFIKI ndani ya CHADEMA... Zitto , Shibuda wahusishwa


Safari yetu ya kubadilisha utawala inaonekana kufika ukingoni na nifuraha ya kila Mtu mwenye hisia ya ukweli katika maisha na ninapotazama mbali sana ninaona jinsi ambavyo Usaliti na Unafiki unavyoangamiza Taifa ni bahati mbaya sana uwezi kuwaepuka katika harakati hizi lakini tukiwa makini tunaweza kuwathibiti .

Kama Chadema leo itashindwa kuwachukulia hatua wasaliti wa wazi wa kazi hii njema ni vipi Chadema itaweza kuitaka Serikali na Rais iwajibishe Viongozi wake katika ufisadi na wizi wa mamilioni ? Na Wananchi lazima wajue lengo kubwa na muhimu la Chadema kwanza liwe kubadilisha fikra na mitazamo na kuupa UMMA elimu na mamlaka na nguvu ya kusimamia Taifa lao katika kuhoji ,kudadisi na kukemea , kwani UMMA usipojua wajibu wake katika kusimamia rasilimali na Taifa lao , ukweli utabaki kuwa Nchi itabadilishwa na kufanikishwa na Jamii iliyoamua kuishi matendo dhahiri ya ukweli na haki na sio unafiki na usaliti .

Viongozi wote wa Siasa wanatokana na Jamii kwa hiyo jamii Thabiti inayo furahia UTU ni Nchi bora tutakayoijenga lakini Jamii yenye woga na hofu na Sifa itazaa Taifa lenye usaliti na Wanafiki . Usaliti na Unafiki unaliangamiza Taifa sana . Maombi na Dua za Watu wengi kuelekea 2015ni kutaka kuona Chadema inachukua Nchi , lakini Dua na Sala hizi zina Imani kubwa na Viongozi wa Chadema na sio rangi ya Chadema , hivyo ni muhimu Chadema kuchukua hatua sasa ya kusafisha Chama na kama hatua hiyo muhimu ya kuondoa Watu wenye rangi mbili italeta madhara katika Uchaguzi Mkuu wa 2015 kwamba tunaweza tusishinde dola basi madhara hayo ni muhimu kwani lengo letu lisiwe tu kwenda Ikulu bali kubadilisha fikra ya utawala katika kutenda na kuamua .

“ Ni bora Simba wakali mia moja walioko Nje kuliko nyoka mdogo mmoja aliye ndani “ Chadema lazima ifanye maamuzi sasa ya kusafisha Nyumba yake la sivyo itakuja kujuta katika siku za mwisho , wasaliti wote waondolewe hasa yule Kiongozi wao kwani hakuna genge la usaliti lisilokuwa na Kiongozi , kuna Watu wengi Vijana wamekuwa wahanga na ndoto zao kupotea katika Siasa kwa sababu waliongozwa vibaya na Kiongozi mkubwa anayeratibu usaliti ndani ya Chama .

Mtu huyu wote tunamjua ni matumaini yangu Usaliti wake sasa utafika kikomo kama Chama kitaamua kuwa na busara za kutosha katika kujenga siku njema zinazokuja . Mtu huyu amefanya mambo mengi mabaya katika Chama yanayohusu usaliti na amewaponza Vijana wengi na kuangamiza ndoto zao kwa sababu ya mambo yake binafsi .

“ To me, the thing that is worse than death is betrayal. You see, I could conceive death, but I could not conceive betrayal.” Malcolm X
Lema Godbless - Mp

No comments :

Post a Comment

Designed By ApexbnewZ