Wednesday, April 02, 2025

Monday, July 28, 2014

Diamond na Lady Jay Dee Washinda Tuzo za AFRIMAMA 2014 zilizofanyika marekani

Kwa mara nyingine Diamond Platnumz ameendelea kuipeperusha vizuri bendera ya Tanzania kimataifa, baada ya kushinda tuzo ya AFRIMMA 2014 (African Muzik Magazine Awards) zilizofanyika July 26, Eisemann Center Richardson, Texas, Marekani. Diamond ameshinda kipengele cha mwanamuziki bora wa kiume Afrika mashariki.
d afrimma
Diamond muda mfupi baada ya kupokea tuzo yake
Mtanzania mwingine aliyeing’arisha Tanzania katika tuzo hizo ni Lady Jaydee, ambaye nae ameshinda tuzo moja ya mwanamuziki bora wa kike Afrika mashariki.
Diamond kupitia Instagram amepost picha akiwa na tuzo yake na kuandika:
“First of all napenda nimshkuru sana Mwenyez mungu, Mama, Family, My management, kipenzi changu, Media, bila kuwasahau nyinyi mashabiki zangu pendwa kwani sikuzote mmekuwa mkinisupport bega kwa bega kwenye shida na raha…Niwashkuru pia Wasanii wenzangu toka nje na ndani ya Tanzania kwani naamini changamoto tunazopeana ndio zimefanya hadi sasa mziki wetu ufikie hapa…hakika tunzo hizi si zangu bali ni za Muziki wa Bongo flavour… Mwisho kabisa nimshkuru Mh Rais Jakaya Mrisho kikwete kwa mchango wake wa kila siku katika sanaa yetu!… Mr President your Son Did it!!!!! #MdogMdogo”.



Naye Lady Jaydee ameandika:
Nashukuru wote mnaokubali kazi zangu, wote mnaosimama na kutetea JayDee bila kusita, nashukuru kwa Tuzo nyingine tena toka AFRIMMA . Wahenga walinena kuwa utavuna ulichopanda, mapenzi tele kwa kila mtu.

Share
d n d afrimma Diamond na Davido baada ya kupokea tuzo zao
Wanamuziki wengine walioshinda ni pamoja na Davido na Flavour wa Nigeria, ambao wamenyakua tuzo mbili kila mmoja.
Nchi ya Nigeria ndio iliyong’ara zaidi kwa kupata jumla ya tuzo kumi, ikifuatiwa na Afrika Kusini ambao wamepata tuzo tano.
Hii ni orodha kamili ya washindi wa AFRIMMA AWARDS 2014
Best DJ Africa 2014- Dj Black (Ghana)

Best African DJ USA 2014 – Dj Josh (Kenya)

Best Video of the Year 2014- Flavour (Nigeria)
Best Male East Africa 2014- Diamond (Tanzania)

Best Male West Africa 2014- Davido (Nigeria)
Best Female East Africa 2014- Lady Jaydee (Tanzania)

Best Female West Africa 2014 – Tiwa Savage (Nigeria)

Best Male Central Africa 2014 – Fally Pupa (Congo)

Best Female Central Africa 2014- Gasha ( Cameroon)

Best Male Southern Africa 2014- Khuli Chana (South Africa)

Best African Group 2014- P-square (Nigeria)

Best Male Diaspora 2014- Fuse ODG (Ghana)

Best Female Diaspora 2014- Les Nubians (Cameroon)

Best Female Southern Africa 2014- Zahara (South Africa)

Best Dancehall Artist 2014 – Timaya (Nigeria)

Best Dance in a Video 2014- Iyanya (Lekwa Ukwu) (Nigeria)

Best Gospel Artiste 2014- Bahati (Kenya)

Best Traditional Artist 2014- Flavour (Nigeria)

Best Newcomer 2014- Stanley Enow (Cameroon)

Best Video Director 2014- Ogopa Dj’s (Kenya)

Music Producer of the year 2014- Dj Oskido (South Africa)

Best Dance Group 2014- Imagineto (Nigeria)

Best Rap Act 2014- Sarkodie (Ghana)

Best Collaboration 2014- Mafikizolo ft Uhuru (Khona) (South Africa)

Song of the Year 2014- Kcee (Nigeria)

Artist of the Year 2014- Davido (Nigeria)

Leadership in Music Award 2014- 2face Idibia

Legendary Award 2014- Yvonne Chaka Chaka

Transformational Leadership Award 2014- Chief Dr. Godswill Akpabio

No comments :

Post a Comment

Designed By ApexbnewZ