Lile bifu linalondelea kati ya mwigizaji Irene Uwoya
na mmiliki wa kampuni maarufu ya magazeti nchini Erick Shigongo
limeshika hatamu mpya baada ya mwigizaji huyo kuendelea kusema yake ya
moyoni kuhusu kile ambacho anakisema kuendelea kuchafuliwa na
mfanyibiashara huyo kupitia magazeti yake hayo.
Kupitia ukurasa wake wa mtandao mmoja wa kijamii Irene ameandika...
“…Ipo siku ntaongea ukweli kuhusu shigongo na ushaid pia
ntatoa...usilo lijua nikama usiku wagiza ndomana atawadanganya wasio na
akili na wasio mjua....ntapgana nae mpaka tone la mwisho la damu yangu
ntasema kila kitu kwanin ananichukia...na ntaweka kila kitu waz....den
wenye akili watajua naongea nin...simuogop atakama atanichafua kiasi
gan...hizo kwangu ni matone yamvua bado mvua yenyewe...I don care
kwaatakae muamin but mwisho wa siku ukweli utaonekana na atataman ardhi
ipasuke......mim irene uwoya sijashawishiwa na mtu wala kulazimishwa
nahaaidi ya kwamba ntaongea…”
Hayo ni maneno ya mwanadada huyu kuhusu kinachoendelea kati ya na Erick Shigongo.
Na sakata zima ndivyo hivi lilivyo

Baada
ya gazeti la Risasi kuandika habari na kudai kwamba msanii na superstar
Irene Uwoya ametiwa mbaroni kwa wizi wa simu aina ya iPhone 5 mwanadada
huyo ameamua kupiga picha ukurasa wa mbele wa gazeti hilo na kuandika
machache juu yake kupitia ukurasa wake wa fb ambapo amedai ana case na
Shigongo ndo maana wameamua kumchafua. Soma alicho andika hapa chini:

No comments :
Post a Comment